Na: Lucas Raphael,Tabora
Mfuko wa maendeleo ya jamii TASAF kupitia mpango wa kunusuru kaya Masikini wilaya ya Sikonge mkoani Tabora imetoa kiasi cha shilingi milioni 412 ikiwa ni awamu ya tatu ya fedha ambazo zimeanza kutolewa kwa kaya Masikini kwa ajili ya kujikwamua kiuchumi.
Mratibu wa TASAF Wilaya ya Sikonge Cloud Nkanwa alitoa maelezo hayo kwa waandishi wa habari katika zoezi la uhawilishaji lililofanyika jana kwa kaya maskini wiayani humo
Alisema kuwa kiasi cha shilingi milioni 412.4 zimelenga kuwanufaisha kaya masikini 5758 wanaoishi katika vijiji 64 vilivyopo kwenye Wilayani hiyo.
Cloud alisema kwamba walengwa wa mpango wa kunusuru kaya Masikini wanatakiwa kuzitumia fedha wanazopata kwa malengo yaliyokuwasudiwa, ikiwemo kuwapeleka watoto klinik ,kuwanunulia wanafunzi sare za shule na mahitaji mengine muhumi ya watoto.
Aidha alisema kwamba wanufaika wa mpango huo kuzitumia fedha hizo katika mambo yenye tija ilikuweza kujiinua kiuchumi.
“Lengo la mpango huu ni kuinua hali ya maisha na kuongeza kipato, kuwajengea uwezo na kunusuru kaya Masikini zilizo katika Mazingira hatarishi, jambo ambalo Serikalini imekuwa ikilifanya kwa wananchi” alisema Cloud Nkanwa
Katika hatua nyingine wanufaika wa TASAF ambao ni Amisa Husein ,Vaines Leonard na Mary Charles wameishukuru Tasaf kwa kuendelea kuwapatia fedha ambazo zimewasadia katika kutatua changamoto mbalimbali za kimaisha .
“Fedha za TASAF zimenisaidia kufanya Biashara ndogondogo, pamoja na kufuga kuku, na kupitia Biashara nimejenga nyumba ya Bati ambayo mwanzo sikuwa nayo” Mnufaika wa TASAF.
Walisema kwamba Fedha hizo zimelenga kuwawezesha kupata mahitaji ya Msingi na fursa za kujijiongezea kipato kwa njia ya uzalishaji Mali kupitia mpango huo wa kunusuru kaya masikini na kwa ajili ya manufaa ya muda mrefu.
mwisho