Home LOCAL NAIBU WAZIRI KATAMBI AFUNGUA KIKAO CHA KUJADILI MATOKEO YA UTAFITI KUHUSU ATHARI...

NAIBU WAZIRI KATAMBI AFUNGUA KIKAO CHA KUJADILI MATOKEO YA UTAFITI KUHUSU ATHARI ZA UVIKO 19 KATIKA SHUGHULI ZA KIUCHUMI ZA VIJANA

Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia (Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Patrobas Katambi akizungumza katika kikao cha Majadiliano kuhusu Utafiti uliofanyika juu ya Atahari za UVIKO – 19 katika shughuli za Kiuchumi za Vijana hii leo Aprili 14, 2022.

Na: Mwandishi Wetu – Dodoma

 

Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Patrobas Katambi leo Aprili 14, 2022 amefungua kikao cha wadau kilichoandaliwa na Shirika la USAID kwa ajili ya kujadili matokeo ya utafiti uliofanyika kuhusu athari za UVIKO – 19 katika shughuli za kiuchumi za vijana. Mkutano huo ulifanyika kwa njia ya mtandao ambao ulishirikisha wadau mbalimbali zikiwemo Wizara zinazo husika na masuala ya vijana Tanzania bara na Visiwani, Wizara ya Kilimo, Viongozi wa serikali kutoka Mkoa wa Iringa na Mbeya pamoja na Shirika la Feed the Future Tanzania.

 

Naibu Waziri Katambi katika Mkutano huo alielezea mikakati ambayo Tanzania imejiwekea katika kuendelea kutoa fursa mbalimbali kwa vijana zitakazo wawezesha kujikwamua kiuchumi. Pamoja na hayo alipongeza juhudi zilizofanyika kupitia mradi “Advancing Youth” ambao umewanufaisha vijana 38,500 na kusaidia kuzalisha ajira 3,650 kwa vijana katika sekta rasmi na isiyo rasmi. 

 

Aliongeza kuwa Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeendelea kutambua mchango wa unaofanywa na wadau mbalimbali katika kukuza ustawi na maendeleo ya vijana nchini. 

 

Aidha, maandiko ya matokeo ya utafiti huo yaliwasilishwa na wataalam mbalimbali walioshiriki katika mkutao huo. Pia vijana walionufaika na mradi wa Inua Vijana “Advancing Youth” waliweza kutoa shuhuda kuhusu manufaa ya mradi huo.

 

MWISHO.

 

 (PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU)

KAZI, VIJANA, AJIRA NA WATU WENYE ULEMAVU
Previous articleMAKAMU WA RAIS ASHIRIKI FUTARI NA KAMATI YA AMANI
Next articleSHILINGI MILIONI 412.4 ZA TASAF KUNUFAISHA ZAIDI YA KAYA 5000- SIKONGE.
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here