Mganga Mkuu wa Serikali Prof. Tumaini Nagu leo amekagua miradi inayotekelezwa katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Kagera na kuangalia hali ya utoaji wa huduma za afya.
Katika miradi hiyo Prof. Nagu amekagua jengo la wagonjwa wa Dharura(EMD), jengo la Mionzi na jengo la wagonjwa mahututi (ICU).
Aidha, Prof. Nagu amewapongeza watumishi wa hospitali hiyo na kuwatia moyo kuendelea kufanya kazi kwa kuzingatia maadili ili kuleta ufanisi katika kuwahudumia wananchi.
Prof. Nagu amefanya ziara ya siku tatu Mkoani Kagera ikiwa ni ziara yake ya kwanza ya kikazi ya kuangalia utayari wa Mkoa huo katika kukabiliana na tishio la ugonjwa wa Ebola ambao kwa sasa uko nchi ya jirani ya Uganda.