Home BUSINESS SERIKALI HAITAPUNGUZA ENEO LA HIFADHI YA MSITU WA MBIWE KWA WANANCHI –...

SERIKALI HAITAPUNGUZA ENEO LA HIFADHI YA MSITU WA MBIWE KWA WANANCHI – MHE.MSANJA

Serikali imesema haitapunguza eneo la Hifadhi ya Msitu wa Mbiwe kwa ajili ya matumizi ya wananchi na shughuli za kiuchumi ikieleza kuwa itaendelea kulihifadhi eneo hilo kwa lengo la kulinda bioanuai zilizopo katika msitu huo.

Hayo yamesemwa leo Bungeni jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja (Mb) , alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Jimbo la Lupa, Mhe. Masache Njelu aliyetaka kujua endapo Serikali inaona haja ya kupunguza eneo la hifadhi ya msitu huo kwa wananchi.

Ameeleza kuwa lengo la kuanzishwa kwa hifadhi hiyo iliyopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Chunya Mkoani Mbeya, ni kulinda vyanzo vya maji vinavyotumika kwa matumizi ya binadamu na wanyamapori.

Aidha, amesema Sheria ya msitu huo inaruhusu shughuli za uchimbaji wa madini ndani ya hifadhi kwa kuzingatia kanuni na taratibu zilizopo.

Previous articleAUWAWA KWA KUPIGWA RISASI NA MAJAMBAZI GEITA
Next articlePROF. NAGU AKAGUA MIRADI YA AFYA KAGERA 
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here