
Rais mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, akiwa na Andrés Iniesta, gwiji wa soka wa FC Barcelona na timu ya taifa ya Spain, walipokutana katika Uwanja wa Ndege wa Casablanca wakijiandaa kuondoka.
Iniesta, ambaye kwa sasa amestaafu soka la ushindani na anaendelea na shughuli za mafunzo na maendeleo ya soka nchini United Arab Emirates (UAE), pia alikuwepo nchini Morocco kushuhudia fainali ya AFCON kati ya Morocco na Senegal.
Kukutana kwao huko kuliakisi mguso wa nadra kati ya historia ya uongozi wa Afrika na urithi wa soka la dunia—kimya, heshima, na mazungumzo mepesi ya wasafiri wa kawaida.





