Home LOCAL WAZIRI MKUU DKT. NCHEMBA AAGIZA SOKO LA MAJENGO LIKAMILIKE KWA WAKATI

WAZIRI MKUU DKT. NCHEMBA AAGIZA SOKO LA MAJENGO LIKAMILIKE KWA WAKATI

WAZIRI MKUU, Dkt. Mwigulu Nchemba, ameagiza kukamilika haraka kwa ukarabati wa soko la Majengo Jijini Dodoma ili kuwawezesha wafanyabiashara wa jiji hilo kunufaika na mradi huo.

Thank you for reading this post, don't forget to subscribe!

Dkt. Nchemba ametoa maagizo hayo leo Alhamisi, Desemba 11, 2025 wakati alipofanya ziara ya kushtukiza kujionea maendeleo ya ukarabati wa soko hilo unaotarajiwa kukamilika Machi, 2026.

Sambamba na hayo, Waziri Mkuu amemuagiza Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma, Dkt. Fredrerik Sagamiko kuhakikisha kwamba wanatoa kipaumbele cha kugawa vizimba kwa wafanyabiashara waliokuwepo awali katika soko hilo.