Home LOCAL UZALISHAJI WA MAJI UMEPUNGUA KUTOKA LITA MILIONI 270 HADI MILIONI 50 KWA...

UZALISHAJI WA MAJI UMEPUNGUA KUTOKA LITA MILIONI 270 HADI MILIONI 50 KWA SIKU

Thank you for reading this post, don't forget to subscribe!

Ofisa Mtendaji Mkuu MAMLAKA ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA), Mhandisi Mkama Bwire, amesema kuwa kwasasa uzalishaji wa maji umepungua kutoka lita milioni 534.6 kwa siku, hadi lita milioni 270, sawa na upufungu wa lita milioni 264.6 kwa siku.

Mhandisi Bwire amebainisha hayo alipokuwa akitoa wasilisho kuhusu mwenendo wa uzalisha na usambazaji maji katika kikao kazi kati ya Mamlaka hiyo na wahariri wa vyombo vya habari, kilichofanyika leo Desemba 12,2025,  Jijini Dar es Salaam.

Amesema kwa sasa mtambo wa Ruvu Chini uliokuwa na uwezo wa kuzalisha maji lita milioni 270 kwa siku, hivi sasa unazalisha maji lita milioni 50 kwa siku huku mtambo wa Ruvu Juu wenye uwezo wa kuzalisha lita milioni 196 sasa unazalishaji wake umepungua na kufikia lita milioni 150.

Aidha, amezitaja sababu za kupungua kwa uzalishaji maji nakupelekea uwepo wa uhaba wa maji katika mikoa ya Pwani na Dar es Salaam, ambazo ni pamoja na kuchelewa kwa mvua za masika, ambapo pia zilinyesha chini ya kiwango  mwezi Machi mwaka huu. 

Sababu nyingine ni kuongezeka kwa shughuli za kibanadamu zikiwepo  kilimo na ufugaji, ndani
ya Bonde la mto Ruvu, sambamba na kuongezeka kwa Joto kutoka nyuzi joto 29-31C hadi nyuzi joto 33.2-34.2 (TMA), hali hii imepelekea kina cha maji kupungua kutokana na sababu mbalimbali zikiwemo maji kupotea kwa njia ya Mvuke.

“Kuchelewa kwa mua za Vuli zilizotarajiwa kunyesha kuanzia Oktoba – Desemba, 2025 na Mto Ruvu kuacha njia yake ya asili kwenye eneo la Kitomondo na kutengeneza mchepuko.

Pamoja na Changamoto zilizopo, DAWASA inaendelea kuchukua hatua madhubuti kukabiliana na upungufu wa maji kwa lengo la kuhakikisha wananchi wote wanaendelea kupata huduma katika uwiano sawa.” amesema Mhandisi Bwire.

Kuhusu hatua za muda mfupi zilizochukuliwa ni kusimamisha vibali vya watumia maji wengine ili kuruhusu DAWASA kupata maji kwa ajili ya matumizi ya binadamu.

Pia DAWASA kwa kushirikiana na Serikali ya Mkoa wa Pwani, Bodi ya Bonde la Wami-Ruvu, inaendelea kufanya doria kwenye eneo la Mto Ruvu kuhakikisha hakuna matumizi mengine ya maji kutoka kwenye mto.

Hatua nyingine zilizochukuliwa ni kuyagawa na kuyasimamia maji kidogo yanayoendelea kuzalishwa kwa uwiano sawa, kudhibiti mivujo ya maji kwa wakati ili kuhakikisha maji kidogo yanayopatikana yaweze kuwafikia wateja pamoja na kutoa elimu ya kuhifadhi maji na matumizi bora ya maji katika kipindi hiki

Wakati hatua zinachukuliwa za mrefu ni kuanza kwa utekelezaji wa Gridi ya maji ya Taifa, ikiwa ni pamoja na kutoa maji Mto Rufiji kuja Mikoa ya Dar es salaam, Pwani na Lindi pamoja na kuongeza uchimbaji wa visima vya uzalishaji maji kwenye maeneo ya pembezoni mwa Mkoa wa Dar es salaamMwito