Home LOCAL DKT. MWIGULU AKAGUA MAENDELEO YA UJENZI WA MADARAJA LINDI.

DKT. MWIGULU AKAGUA MAENDELEO YA UJENZI WA MADARAJA LINDI.

Asisitiza Rais Dkt. Samia amedhamiria kushughulika kwa vitendo na umasikini wa watanzania_

Thank you for reading this post, don't forget to subscribe!

WAZIRI MKUU, Dkt. Mwigulu Nchemba leo Desemba 19, 2025 amekagua maendeleo ya ujenzi wa Madaraja na Ukarabati wa barabara kuu ya Marendego-Nangurukuru-Lindi-Mingoyo

Akizungumza baada ya ukaguzi huo, Mheshimiwa Dkt. Mwigulu amewaambia wakazi wa Somanga mkoani Lindi kuwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan anatekeleza miradi ya kimkakati ili kushughulika kwa vitendo na umasikini wa Watanzania

Amesema kuwa Rais Dkt. Samia alisimamia ukamilishaji wa Bwawa la Kuzalisha Umeme la Julius Nyerere ili kuhakikisha kila mtanzania ananufaika na huduma ya nishati ya umeme.

“Tumeshuhudia Rais Dkt. Samia namna anavyotekeleza miradi kwenye sekta mbalimbali ikiwemo uvuvi, maji, kilimo, afya, elimu na hata uwezeshaji wananchi kiuchumi”