
Dar es Salaam Tanzania 1 Desemba 2025: Exim Bank Tanzania imezindua kampeni mpya ya matumizi ya kadi katika msimu wa sikukuu iitwayo Chanja Kijanja Dili Ndio Hili inayodumu kwa miezi miwili kuanzia 1 Desemba 2025 hadi 31 Januari 2026 ikiwa na lengo la kuhamasisha matumizi ya malipo yasiyotumia fedha taslimu na kuwazawadia wateja wanaotumia kadi za Exim Mastercard kupitia mashine za POS na mifumo ya malipo mtandaoni katika kipindi cha ongezeko la ununuzi wa sikukuu
Akizungumza wakati wa uzinduzi Mkuu wa Kitengo cha Wateja Binafsi wa Benki ya Exim Andrew Lyimo alisema kampeni hii inaonesha dhamira ya benki kutoa huduma rahisi na salama kwa wateja wanaotumia malipo ya kidijitali
“Kupitia Chanja Kijanja Dili Ndio Hili tunataka kufanya malipo ya kila siku kuwa rahisi zaidi huku tukiwapa wateja fursa ya kushinda zawadi mbalimbali katika msimu huu wa sikukuu Mpango huu unaakisi kujitoa kwetu kukuza utamaduni wa malipo ya kidijitali na kuboresha uzoefu wa wateja kote nchini” alisema
Wateja watakuwa na nafasi ya kujishindia zawadi mbalimbali zikiwemo
Zawadi za kila wiki: Wateja watano 5 kujishindia Sh100000 kila mmoja
Zawadi za kila mwezi: Wateja kumi 10 kujishindia Sh200000 kila mmoja
Siku maalum za Cashback: Wateja kurejeshewa fedha kulingana na thamani ya miamala yao katika tarehe hizi
Black Friday – 28 Novemba 2025
Cyber Monday – 1 Desemba 2025
Siku ya Krismasi – 25 Desemba 2025

Zawadi kubwa mwisho wa kampeni: Sh milioni 5 Sh milioni 10 na zawadi kuu ya Sh milioni 15
Mkuu wa Kitengo cha Mifumo Mbadala na Mabadiliko ya Kidijitali wa Exim Silas Mtoi alisema kampeni hii inalenga kubadili namna Watanzania wanavyopata huduma za malipo ya kidijitali
“Kampeni hii ni zaidi ya zawadi Inalenga kuwafanya wateja wajisikie urahisi kasi na usalama wa kutumia kadi kila wanapolipa iwe dukani au mtandaoni Kwa kuongeza matumizi ya kadi tunachochea safari ya kuelekea uchumi usio na matumizi makubwa ya fedha taslimu Hii si kampeni ya msimu huu pekee bali ni hatua muhimu kuelekea Tanzania yenye kujiamini kidijitali” alisema
Wateja wanaotumia kadi za Exim pia watapata zawadi maalum wanaponunua katika maduka ya Shoppers na Village Supermarket pamoja na punguzo la msimu katika maeneo mbalimbali ya chakula na burudani ikiwemo Karambezi Café na CIP Lounge uwanjani

Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mawasiliano wa Benki ya Exim Stanley Kafu alisema kampeni hii imeandaliwa kwa ajili ya kuthamini wateja katika msimu wa sikukuu
“Kampeni hii ni njia yetu ya kusherehekea na wateja msimu huu Iwe ni manunuzi ya sikukuu maandalizi ya sherehe za familia safari ujazaji mafuta chakula cha Krismasi na Mwaka Mpya kulipia ada za shule au kufuatilia ofa za mtandaoni kila ulipaji kwa kutumia kadi ya Exim unakupa urahisi na usalama pamoja na nafasi ya kushinda msimu wote” alisema
Aliongeza kuwa kampeni hii imetengenezwa kwa kuzingatia mahitaji ya wateja hususan usalama wa malipo urahisi na thamani ya zawadi katika kipindi chenye changamoto za kifedha
Kafu pia alibainisha umuhimu wa kampeni katika mpango wa mabadiliko ya kidijitali wa benki akisema inaongeza kasi ya matumizi ya kadi na kuchochea safari ya nchi kuelekea mifumo ya malipo ya kidijitali
Mwakilishi kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania aliipongeza Exim Bank kwa kuendesha kampeni inayolenga wateja na kusimamia uwazi Alisema Bodi itasimamia kwa karibu mchakato wa droo ili kuhakikisha haki na uwazi kwa washiriki wote wanaokidhi vigezo
Kadri matumizi ya malipo ya kidijitali yanavyozidi kukua nchini Exim Bank inalenga kuongeza matumizi ya kadi kupunguza hatari za utunzaji wa fedha taslimu na kuimarisha mfumo wa kifedha unaofanya kazi kwa ufanisi zaidi Benki inawahimiza wateja kushiriki na kunufaika na zawadi msimu huu wa sikuku.





