
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila, ametoa wito kwa wananchi kudumisha amani na kulinda miundombinu ya mafuta akisema jiji hilo ni moyo wa uchumi wa taifa, hivyo vurugu au uharibifu wowote huathiri maisha ya Watanzania wengi.
Amesema Serikali ipo bega kwa bega na wadau wa mafuta kuhakikisha biashara hizo zinaendelea kwa usalama huku elimu ikiendelea kutolewa kwa wauzaji kuhusu uuzaji salama wa mafuta hasa kwa wanaohudumia boti, minara na jenereta kupitia njia za madumu.





