Home LOCAL WASIRA AWAPA UJUMBE MZITO WALIOONGOZA UBUNGE, UDIWANI

WASIRA AWAPA UJUMBE MZITO WALIOONGOZA UBUNGE, UDIWANI

Thank you for reading this post, don't forget to subscribe!

MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara, Stephen Wasira wanachama walioongoza kura za maoni na kupewa dhamana ya kupeperusha bendera ya Chama katikabuchaguzi mkuu wa mwaka wana dhima ya kuwaunganisha wana CCM na na sio kuwafarakanisha.

Amesema CCM ni kama mtumbwi unaosafiriwa na wengine, hivyo haitavumiliwa kuona watu wachache wanataka kuutoboa kwa utazamisha watu wote.

Wasira alieleza hayo kilosa mkoani Morogoro alipokuwa akizungumza na wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM ya wilaya hiyo, akiwa katika ziara ya kutafuta kura za mgombea urais wa CCM, wagombea ubunge na udiwani.

Alisema anatambua kuna msuguano, kwenye baadhi ya kata ambapo walioshindwa wanasema hawajashindwa vizuri, hivyo kusababisha misuguano na walioshinda.

“Sisemi hapa mna matatizo makubwa, wala sikweli, yako majimbo yana matatizo nimepitapita huko nimekutana na matatizo makubwa, kuna mahali imenibidi nifanye maamuzi magumu, lakini hapa ninaambiwa matatizo hayo yapo lakini yanaweza kumalizwa.

“Sasa ushauri wangu au niagize kwa wale walioshinda, nyinyi mnadhamana zaidi ya kuleta umoja kuliko walioshindwa, kwa sababu ukishinda na wewe tena ukawa unatamba na watu wako nao wanawatambia wengine, unatufarakanisha,” alisema.

Makamu Mwenyekiti Wasira alisema ushindi walioupata baadhi ya wana CCM kwa kuongoza kura za maoni unatokana na mfumo iliyojiwekea Chama kupata wagombea.

Ule ushindi wa ndani ya Chama ni mfumo wa kupata mgombea siyo mapambano ya kufanya wengine waonekane wanafaa na wengine waonekane hawafai, sio kweli. Maana kuna mahali pengine hata aliyeongoza hatukumchukua tukamchukua wa pili, kuna mahali tukamchukua wa tatu,” alisema.

Aliwasihi waliopewa nafasi kuonyeshe njia katika kuleta umoja muende kwa walioshindwa kwa kuwa nyinyi na wao ni wanachama wa CCM na uongozi ni zamu kwa zamu, hivyo kama ilikuwa zamu yenu kuongoza basi ambao hawakuongoza na wao zamu yao itakuja.

CCM sisi ni kama watu tunasafiria kwenye mtumbwi sasa usitoboe lmtumbwi ambao tunasafiria wote, maana ukiutoboa tunazama wote, hapana kutoboa mtumbwi tunaosafiria, mtumbwi wa kudumu tunasafiria wote, kwa hiyo ukiongoza leo utaongoza kwa miaka mitano, mtumbwi ule utakuwa bado upo kwa wengine nao kusafiria.

Wale ambao hawakufanikiwa wako hapa, jana nilikuwa nao wale wa Kilosa, hapa nao wapo tena vijana tu, ambao baada ya miaka mitano watakuwepo, kwa hiyo nyinyi mliotangulia msije mkadhani hawa hawapo, wapo, wapo wanaangalia nyinyi mnaendeleaje, mnaendeshaje mtumbwi na wao nawashukuru sana sana kwa kuja mbele,” alisema.

Katika ziara hiyo wasira alimwombea kura Mgombea urais kupitia CCM, Dk. Samia Suluhu Hassan, mgombea ubunge Jimbo la Kilosa Profesa Palamagamba Kabudi, mgombea ubunge Jimbo la Mikumi, Denis Londo, pamoja na wagombea udiwani katika majimbo hayo.