1. Mwenyekiti wa Baraza la
Wafanyakazi wa TEA Dkt. Erasmus Kipesha akisisitiza jambo katika kikao cha tano
kilichofanyika mjini Morogoro Septemba 11 na 12, 2025. Kulia ni Katibu msaidizi
Bw. Lusungu Kaduma.
:::::::::::
Watumishi wa Mamlaka ya Elimu Tanzania
(TEA) wamekutana kwa siku mbili mkoani Morogoro katika kikao cha Baraza la
Wafanyakazi kujadili utekelezaji wa shughuli za Mamlaka kwa mwaka wa fedha
2024/2025 pamoja na kuwasilisha na kuchambua mpango kazi wa mwaka 2025/2026.
Kikao hicho cha siku mbili kilichoanza
Septemba 11 hadi 12, 2025 kimeongozwa na Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi
ambaye pia ni Mkurugenzi Mkuu wa TEA, Dkt. Erasmus Kipesha.
Katika kikao hicho, wajumbe walipata fursa
ya kupokea taarifa za utekelezaji kutoka kwa vitengo mbalimbali vya Mamlaka, na
kutoa maoni na mapendekezo ya namna ya kuboresha utekelezaji wa majukumu kwa
ufanisi zaidi.
Akizungumza wakati wa kufungua kikao hicho,
Dkt. Kipesha alieleza kuwa Baraza la Wafanyakazi ni jukwaa muhimu
linalowawezesha watumishi kushiriki moja kwa moja katika upangaji wa mipango na
utekelezaji wa majukumu ya taasisi.
Alisisitiza kuwa ushiriki wa watumishi
katika kujadili utekelezaji wa majukumu ya mamlaka na mikakati iliyowekwa
kwenye utekelezaji ni msingi wa uwajibikaji, ufanisi na mafanikio ya taasisi
kwa ujumla.
“Mkutano huu ni fursa mahsusi ya
kujitathmini, kubadilishana mawazo, na kupanga kwa pamoja mikakati ya
kuimarisha utendaji wetu ili kufanikisha malengo ya Mamlaka,” alisema Dkt.
Kipesha.
Katibu wa Baraza la Wafanyakazi
wa TEA Bi. Mwanaisha Komba akitoa maelezo kwa wajumbe wa baraza hilo katika
kikao cha tano kilichofanyika mjini Morogoro kwa lengo la kujadili taarifa
mbalimbali za utekelezaji na kiutumishi.
Kaimu Mkurugenzi UtafutatajiRasilimali na Usimamizi Miradi ya Elimu Bw. Masozi Nyirenda akitoa ufanunuzi
kuhusu utekelezaji wa miradi ya elimu kwa wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa
TEA mjini Morogoro.
1. Mkurugenzi wa Huduma za Taasisi
CPA. Mwanahamis Chambega akitoa maelezo kuhusu utekelezaji wa bajeti ya mamlaka
kwa wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa TEA katika kikao cha tano
kilichofanyika mjini Morogoro.
1. Meneja Huduma za Sheria kutoka
Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA), Bi. Christina Meela (katikati)akitoa taarifa
ya utekelezaji kwa wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa TEA katika kikao
kilichofanyika mjini Morogoro.
1. Mkaguzi Mkuu wa Ndani CPA.
Richard Mazinge akitoa maelezo kwa wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa TEA
kwenye kikao cha tano kilichofanyika mjini Morogoro kwa lengo la kupitia na
kujadili taarifa mbalimbali za utekelezaji za mamlaka. Kushoto ni Mkurugenzi wa
Huduma za Taasisi CPA. Mwanahamis Chambega.
1. Kaimu Meneja Usimamizi wa
Miradi ya Elimu Bi. Mwafatma Mohamed akijibu maswali ya wajumbe wa Baraza la
Wafanyakazi wa TEA walipokutana mjini Morogoro kupitia na kujadili taarifa za
utekelezaji wa majukumu ya mamlaka hiyo.
1. Baadhi ya wajumbe wa Baraza la
Pili la Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) wakifuatilia uwasilishwaji wa taarifa
za utekelezaji katika kikao cha tano cha baraza hilo kilichofanyika mjini
Morogoro.
1. Mwenyekiti wa Baraza la
Wafanyakazi wa TEA Dkt. Erasmus Kipesha (kulia) pamoja na Katibu wa Baraza hilo
Bi. Mwanaisha Komba (kushoto) wakifuatilia taarifa na maoni kutoka kwa wajumbe
wa baraza hilo wakati wa kikao cha tano kilichofanyika Morogoro.
1. Baadhi ya wajumbe wa Baraza la
Pili la Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) wakifuatilia uwasilishwaji wa taarifa
za utekelezaji katika kikao cha tano cha baraza hilo kilichofanyika mjini
Morogoro.
1. Wajumbe wa Baraza la Pili la
Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA), wakiwa katika picha ya pamoja walipokutana
kwenye kikao cha tano cha baraza hilo Morogoro.
1. Baadhi ya wajumbe wa Baraza la
Pili la Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) wakifuatilia uwasilishwaji wa taarifa
za utekelezaji katika kikao cha tano cha baraza hilo kilichofanyika mjini
Morogoro.
http://TEA YAJADILI UTEKELEZAJI WA SHUGHULI NA MPANGO KAZI MPYA KUPITIA BARAZA LA WAFANYAKAZI




.jpeg)

.jpeg)

.jpeg)

.jpeg)




