MGOMBEA Mwenza wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dk. Emmanuel John Nchimbi, akiwasalimia Wanachi wa kata ya Katumba,Halmashauri ya ya Nsimbo leo Jumatano Septemba 10,2025, wakati akielekea Wilaya ya Mlele katika Jimbo la Kavuu, kuhutubia Wananchi kwenye mkutano wake mkubwa wa hadhara wa Kampeni mkoani Katavi.
Baada ya kuwasalimia Wananchi wa Nsimbo, Dkt. Nchimbi aliwanadi Wagombea Ubunge wa majimbo mbalimbali ya Mkoa huo,akiwemo mgombea Ubunge wa jimbo la Nsimbo,Anna Richard Lupembe pamoja na Madiwani.
Dkt. Nchimbi ameendelea kunadi Ilani ya CCM ya Uchaguzi Mkuu 2025-2030,ambayo kimsingi imelenga kwenda kuboresha maisha ya wananchi na ustawi wa Maendeleo katika miaka mitano ijayo.
Aidha amekuwa akitumia nafasi hiyo kuwaomba wananchi kumchagua mgombea Urais wa CCM,Mhe.Dkt Samia Suluhu Hassan, Wabunge na Madiwani wa Chama hicho kwa kura za kishindo ifikapo Oktoba 29,2025
http://DKT.NCHIMBI ASIMAMA KUWASALIMIA WANANCHI WA NSIMBO AKIELEKEA WILAYA YA MLELE -KATAVI