Monduli Juu, Arusha, 15 Agosti 2025. Tanzania Breweries Plc (TBL), mshiriki muhimu katikamnyororo wa thamani wa kilimo nchini Tanzania, imechukua hatua madhubuti kuimarisha
kilimo cha shayiri nchini kwa kukutana na wakulima wa Monduli Juu, Arusha, na kuwapatia
mafunzo ya vitendo pamoja na ushauri wa kitaalamu wenye lengo la kuongeza mavuno na
kuboresha ubora wa zao. Kikao hiki cha kubadilishana maarifa kimefanyika wakati wa Siku ya
Wakulima wa Shayiri, hafla inayoongozwa na viongozi wa serikali za mitaa na uwepo wa
Katibu wa Wilaya ya Monduli, Mheshimiwa Muhsin Kassim. Tukio hili limewaleta pamoja
wakulima 200, viongozi wa jamii, na wadau wa sekta ya kilimo kujadili suluhu za kufanikisha
ukuaji endelevu wa uzalishaji wa shayiri.
Hafla hii ya kila mwaka imekuwa jukwaa la kutambua na kuthamini mchango wa wakulima
hodari katika usambazaji wa shayiri nchini. Pia imesisitiza dhamira ya serikali kuendelea kuunga
mkono sekta ya kilimo kama mhimili wa ukuaji wa uchumi, hasa katika mikoa kama Arusha
ambako kilimo cha shayiri kimekuwa chanzo cha kipato na ajira kwa maelfu ya kaya.

Akizungumza katika hafla hiyo, Katibu Tawala wa Wilaya ya Monduli, Mheshimiwa Muhsin
Kassim, amewaeleza wakulima kuhusu juhudi za serikali katika kuongeza tija, upatikanaji wa
pembejeo, na upanuzi wa masoko ya shayiri na mazao mengine muhimu. “Wakulima ndiyo uti
wa mgongo wa taifa letu. Leo tunasherekea kazi zao na tunathibitisha upya dhamira yetu
ya kuwasaidia kupitia utafiti, huduma bora za ugani, na upatikanaji wa masoko yenye tija,”
alisema.
Tanzania Breweries Plc (TBL), mmoja wa wanunuzi wakubwa wa shayiri inayolimwa hapa
nchini, ilishiriki katika hafla hiyo na kutoa shukrani kwa wakulima wanaowauzia zao hili
muhimu, kwa kuwapa ujuzi wa kipekee utakaowasaidia kuboresha uzalishaji. Shayiri ni
malighafi ya msingi katika shughuli za utengenezaji wa bia wa TBL, na kwa miaka mingi
kampuni imekuwa ikiunga mkono wakulima wadogo kupitia mikataba salama ya mauzo pamoja na mafunzo ya kilimo bora.

Akizungumza katika hafla hiyo, Mkurugenzi wa maswala ya sheria na mahusiano ya kampuni
ya TBL, Bi. Neema Temba amesisitiza msimamo wa kampuni kuendelea kununua mazao kutoka
ndani ya nchi na kuwawezesha wananchi kupitia ushiriki shirikishi wa kiuchumi. “Matukio kama
haya yanatukumbusha nafasi muhimu ya wakulima siyo tu katika usalama wa chakula, bali
pia katika kuendeleza viwanda kama chetu. TBL tumejikita katika kuimarisha uhusiano na
wakulima na kuunga mkono kilimo endelevu kinachowanufaisha wote katika mnyororo wa
thamani,” alisema.
Hafla hiyo ilihusisha Shamba Darasa na vipindi vya kubadilishana maarifa. Pia ilitumika kama
jukwaa la kujadili changamoto zinazokumba ekosistimu ya shayiri ikiwemo mabadiliko ya
tabianchi, upotevu wa mazao baada ya mavuno, na upatikanaji wa pembejeo bora, pamoja na
kutafuta suluhu za pamoja kwa siku zijazo.
Siku ya Wakulima wa Shayiri ilihitimishwa kwa wito wa pamoja kutoka kwa wadau wote wa
sekta hii kuimarisha zaidi ushirikiano kati ya sekta binafsi, wakulima, na taasisi za serikali ili
kuongeza tija, uendelevu, na upatikanaji wa masoko kwa wakulima katika mnyororo wa
thamani wa shayiri.
TBL pia ni biashara endelevu iliyo na dhamira ya kuhamasisha na kuwawezesha wateja wake
kujenga Dunia Bora. Hii ni kwa sababu kujenga dunia bora ni jukumu linalowezekana tu pale
tunaposhirikiana, hata kama tupo mbali mbali.




