
Aliyekuwa Mbunge wa Viti Maalum kupitia Chama cha Mapinduzi CCM mkoa wa Iringa, Rita Kabati, ameibuka kidedea katika kura za maoni, kupeperusha bendera ya Chama hicho kugombea kiti cha Ubgunge jimbo la Kilolo Mkoani humo.
Kabati ameibuka mshindi wa kwanza dhidi ya wenzake sita kwa kupata kura 4,565, akimuacha mpinzani wake wa karibu Novat Mfalamagoha aliyepata kura 3,845 ikiwa ni tofauti ya kura 720.
Wengine walioshiriki mchakato huo, ni Nathani Mnyamani aliyepata kura 1,993, huku Festo Kipale akipata kura 1,352.
Pia kwenye mchakato huo, Ndug. Shamidi Nzogela ameshika nafasi ya tano kwa kura 1,111 na Mwalubadu Ngaga akishika nafasi ya mwisho kwa kupata kura 137.




