Home LOCAL NAWANDA ASHIKWA PABAYA NEWALA

NAWANDA ASHIKWA PABAYA NEWALA

Thank you for reading this post, don't forget to subscribe!

Na Mwandishi Wetu

MGOMBEA Ubunge Jimbo la Newala Vijijini kupitia Chama cha Wananchi (CUF), Mneke Jafari, amshika pabaya mgombea Ubunge kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM)Nawanda Yahaya kwa kudanganya Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC)

Mneke ameweka pingamizi kwa Nawanda baada ya kushindwa kuiambia ukweli INEC kuhusu tuhuma za Kesi ya ulawiti na unyanyasaji wa kijinsia ililiokuwa ukimkabili siku chache zilizopita.

Mneke amemwekea pingamizi Nawanda kwa kutoa taarifa za uongo kuwa hajawahi kushitakiwa kwa kosa la jinai.

Katika pingamizi lake kwenda INEC Mneke amedai kuwa Nawanda katika fomu ya uteuzi ya wagombea ubunge sehehu A inayohusu taarifa binafsi za mgombea ubunge, swali namba 13 lenye Sehemu mbili 2 linauliza.

Je, umewahi kushtakiwa kwa kosa la jinai na makosa ambayo ilishitakiwa.

Mneke alisema kupitia swali hilo Nawanda ameidanganya INEC na kwenda kinyume na kiapo cha Mahakama kwa kutoa taarifa za uongo kuwa hajawahi kushtakiwa kwa kosa la jinai.

Mneke ameileza INEC kupitia Fomu Na 9B ya pingamizi kuwa, Nawanda ametoa raarifa ya uongo, ukweli ni kuwa Nawanda ameshawahi kushtakiwa kwa Mahakama ya Mfawidhi kwa kosa la Jinai la Ulawiti na Unyanyasaji.

Aidha, Mneke amechukua hatua zaidi za kulipeleka shauri hilo Tume Huru ya Uchaguzi INEC kupitia fomu Namba 12 ya Rufaa.

Mneke, ameiomba INEC kutengua uteuzi wa Nawanda kwa sababu amepoteza sifa za mgombea kwa kitendo chake cha kutoa taarifa za uongo katika fomu yake ya Umuteuzi.