Home LOCAL TEF YAMPONGEZA Dkt. KAALE KUCHAGULIWA MW.KITI MPYA TAMWA

TEF YAMPONGEZA Dkt. KAALE KUCHAGULIWA MW.KITI MPYA TAMWA

Thank you for reading this post, don't forget to subscribe!

JUKWAA la Wahariri Tanzania (TEF), linampongeza Dk. Kaanaeli Kaale kwa kuchaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Chama cha Wanahabari Wanawake Tanzania (TAMWA).

Uchaguzi huu ni ushuhuda wa imani kubwa waliyonayo wanahabari wanawake kwake kutokana na mchango wake thabiti katika tasnia ya habari.

TEF inaamini kuwa chini ya uongozi wa Dk. Kaale, TAMWA itaendelea kuwa sauti imara ya kupigania usawa wa kijinsia, haki za wanawake na ustawi wa wanahabari nchini,

TEF inaahidi kuendeleza ushirikiano kwa TAMWA, huku ikimtakia kila la heri Dk. Kaale katika majukumu yake mapya.

Pia tunampongeza Mwenyekiti aliyemaliza muda wake, Joyce Shebe kwa kuifikisha TAMWA kwenye mafanikio makubwa.

Mungu aendelee kuijaalia kila la heri tasnia ya habari nchini.

JUKWAA LA WAHARIRI TANZANIA

Deodatus Balile
Mwenyekiti
29/06/2025