Home LOCAL TANZANIA MWENYEJI KONGAMANO LA 18 LA E-LEARNING AFRIKA

TANZANIA MWENYEJI KONGAMANO LA 18 LA E-LEARNING AFRIKA

Thank you for reading this post, don't forget to subscribe!

Na Lilian Ekonga –  DAR ES SALAAM

Tanzania inatarajia kuwa mwenyeji wa Kongamano la 18 la kimataifa la e-Learning Afrika ambalo hufanyika kila mwaka kwa lengo la kujadili utekelezaji wa ajenda ya kuimarisha ukuaji wa Sekta ya elimu Barani Afrika.

Akitoa Taarifa hiyo kuelekea kwenye Kongamano hilo litakalo fanyika Mei 7 hadi 9 mwaka huu, Mkurugenzi wa Sayansi, Teknolojia na Ubunifu kutoka Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa, Ladislaus Mnyone, amesema kufanyika kwa Kongamano hilo ni sehemu ya utekelezaji wa ajenda ya kukuza Sekta ya elimu katika Bara la Afrika.

Amesema kongamano hilo linatarajiwa kukutanisha Mawaziri 20 na Viongozi mbalimbali kutoka ncbi za Afrika pamoja na Washiriki takribani 1300, huku watanzania wakiwa 500.

“Lengo la kuongamano hili ni kuleta wadau kutoka kwenye makundi mbalimbali ikiwemo Wataalamu, Wafanayabisahara, Wawekezaji, Watafiti pamoja na Wabunifu, kujadili na kupanga mikakati ya pamoja kama Bara la Afrika, ya namna gani tutachagiza maendeleo ya matumizi ya tekenolojia ya kidigital kwenye ya Elimu” amesema

Ameongeza kuwa Kauli mbiu ya Kongamono hilo ni ‘Kufikiria upya Elimu na Rasimali watu kwaaajili ya Ustawi wa Afrika’ huku mada mbalimbali kizijadiliwa katika maeneo tofauto na kuona kwa namna gani Elimu itaweza kuzalisha zaidi rasimali watu, na kuongeza maendeleo na matumizi ya kidigitali.

“Kwenye kongamano hili kutakuwa na mijadala kuhusu masuala ya teknolojia za kidigital, Mikutano ya Mashirikano, na kutengeneza mashirikiano baina ya nchi na nchi, Mashirika na Makampuni binafsi, Pia kutakuwa na mkutano wa Mawaziri” ameongeza.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Tehama Wizara ya elimu, Lina Rujweka amesema kwenye kongamano hilo wamealika wabunifu mbalimbali ambao wataonesha bunifu zao ambazo zitasidia katika sekta ya Elimu

“Tumealika wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar, TAMISEMI, Mamlaka ya Serikali Mtandao, Wizara ya AFya na Wizara ya Fedha, hawa wote watakuja kuonesha Teknolojia Bunifu ambazo tunazo” amesema Rejweka

Nae Samson Sitta, Afisa Programu Milele Zanzibar Foundation amesema wamesikia fahari sana kujumuika kwenye kongamana hilo, kwa lengo la kujifunza kutoka kwenye mataifa mengine, na kuonesha bunifu mbalimbali ambao tanzania twanaweza kubuni