Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan pamoja na viongozi wengine wa Serikali, wakishiriki katika ibada maalumu ya mazishi ya aliyekuwa Makamu wa Kwanza wa Rais na Waziri Mkuu Mstaafu, Hayati Cleopa David Msuya, katika Kanisa la KKKT Kristo Mchungaji Mwema; Dayosisi ya Mwanga, Jimbo la Kaskazini, Usharika wa Usangi Kivindu, mkoani Kilimanjaro, leo Mei 13, 2025.