Na. Mwandishi Wetu
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI na Mbunge wa Rufiji Mhe. Mohamed Mchengerwa, ameshuhudia hafla ya utiaji saini mikataba ya ujenzi wa miradi ya Maji itakayojengwa katika Vijiji vitatu vya Mloka, Mbunju Mvuleni pamoja na Ndundutawa ambayo itahudumia Wananchi 16, 593 hali itakayosaidia kupunguza kero ya Maji katika maeneo hayo.
Meneja wa Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) Wilayani Rufiji Mhandisi Alkam Sabuni, alisema ujenzi wa Miradi ya Maji katika Vijiji hivyo utagaharimu kiiasi cha Shilingi 791,068,682.56.
“Katika Kipindi Cha Mwezi Juni 2025 hadi Oktoba 2025 Wananchi wapatao 16,593 wa Vijiji vitatu vya Mloka, Mbunju Mvuleni na Ndundutawa wanaenda kunufaika na huduma ya Maji safi na salama na yenye kutosheleza, ambapo miradi hii itakapokamilika itaongeza hali ya upatikanaji wa Maji kutoka asilimia 86.6 ya sasa hadi asilimia 97.3” alisema Sabuni
Hafla ya Utiaji Saini wa Mikataba ya ujenzi wa miradi hiyo imefanyika katika Kijiji Cha Mloka Kata ya Mwaseni Jana Mei 6, 2025.
Sabuni aliongeza kuwa RUWASA Wilayani Rufiji inatoa huduma katika Vijiji 38 vyenye Jumla ya Watu 157,412 kwa Mujibu wa Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2022.
Kwa upande wake Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe. Mohamed Mchengerwa alisema uwepo wa miradi iyakapokamilika itasaidia kupunguza adha ya Wananchi kwenda kuchoma Maji katika Mto Rufiji.
“leo tumeandika historia katika changamoto ambazo tumekuwa tukizipata kwa muda mrefu leo tumezimaliza na matarajio yangu kwamba Mkandarasi sasa ataanza kazi mara Moja” alisema Mchengerwa.
http://KERO YA MAJI KIJIJI CHA MLOKA, MBUNJU MVULENI NA NDUNDUTAWA YAPATIWA UFUMBUZI