Na Ferdinand Shayo ,Killimanjaro.
Kampuni ya kuzalisha vinywaji changamshi ya Mati Super Brands Limited imejipanga kudhamini na kushiriki mashindano ya West Killi Tour Challenge 2025 yatakayofanyika katikati ya hifadhi ya shamba la miti la West Kilimanjaro Juni 21 jadi 22 mwaka huu wilayani Siha mkoani Kilimanjaro ambapo mamia ya wanamichezo watashiriki kwenye michezo mbali ikiwemo riadha,mbio za baiskeli na piki piki .
Meneja Mauzo na Masoko wa kampuni ya Mati Super Brands Limited mkoa wa Kilimanjaro Brayson Mnene amesema kampuni hiyo imekua ikishiriki na kudhamini michezo mbali mbali,Sanaa pamoja na kutoa misaada kwa jamii inayowazunguka.
Mnene amesema kuwa wateendelea kuunga mkono juhudi za serikali katika kuhifadhi mazingira katika hifadhi ya Shamba la miti la West Kilimanjaro na kukuza utalii wa michezo.
Mhifadhi wa Shamba la Miti la West Kilimanjaro Robert Faida amepongeza wadau wote waliojitokeza kuunga mkono mashindano hayo yanayolenga kutangaza vivutio vya utalii vinavyopatikana ikiwemo maporomoko ya maji,wanyamapori na miti ya asili.
Mkuu wa Wilaya ya Siha Chritopher Timbuka amewataka watanzania kujitokeza kwenye mashindano hayo na tayari maandalizi makubwa yamefanyika ili kufanikisha tukio hilo kubwa.