Home LOCAL TAMASHA LA KUOMBEA UCHAGUZI KUFANYIKA JUNI 2025

TAMASHA LA KUOMBEA UCHAGUZI KUFANYIKA JUNI 2025

Mkurugenzi wa Msama promotion na Muandaaji  wa Tamasha la Kuombea Uchaguzi Alex Msama amesema tamasha la Kuombea Uchaguzi Mkuu litafanyika tarehe 21 june 2025 jijini Dar es slaaam.
Akizungumza na waandishi wa habari Aprili 13, 2025, Msama amesema tamasha hilo litaanzia jijini Dar es salaam na kuzunguka mikoa mingine 25.
Amesema Tamasha hilo ni sehemu nzuri ya kuliombea Taifa kubaki salama hasa kwa viongozi wetu kwa kuwaombea ili kupata viongozi ambao wametoka kwa Mungu.
“Tunaendelea kuongea na waimbaji wa mataifa mablimbali na waimbaji tukota afrika kusini tumeshakubaliana, waimbaji kutoka nigeria tumeshakubaliana, Rwand tupo na mazungumzo nao na waimbaji wa ndani wanasubiri siku ya tarehe husika” amesema Msama
Ameongeza kuwa Bado wanahitaji wadhamini wa kutosha kutokana na gharama mbalimbali za waimbaji wanaotoka nje ya nchi kama Nigeria, Afrika Kusini, Rwanda, Congo, Nigeria wanapo kuja nchini.
Kwa upande wake Philip Mwotsi Mchungaji kutoka kanisa FPCF, amesema Maombezi hayo ni sehem muhimu ambayo inaweza kufanya taifa liwe salama na wakiombea viongozi watapa viongozi ambao wametoka kwa Mungu.
“Watanzania tuungane tumuombe Mungu kuelekea uchaguzi Mkuu ili uchaguzi uende salama, wito wangu kwa wabab na wamama kujitokeza kwa wingi katika Tamasha la Maombezi tukamuombe Mungu kuiombea Nchi na katika umoja inawezekanaa” amesema Rose David, Mchungaji kutoka kanisa la Pentekoste