Akagua miradi lukuki jimbo la Ubungo na kufanya Mkutano wa hadhara viwanja vya TP-Sinza.
Mkuu wa Mkoa wa Dar ea salaam Mhe Albert Chalamila amemtaka mkandarasi anaefanya upanuzi wa barabara ya Morogoro kuanzia eneo la ubungo mataa hadi kimara kuongeza kasi ya ujenzi wa barabara hiyo ili kupunguza adha ya msongamano wa magari kwa wananchi
RC Chalamila ameyasema hayo leo April 10,2025 jijini Dar es salaam ikiwa ni siku ya pili ya ziara yake Wilaya ya Ubungo ambapo ametembelea miradi mbalimbali ya maendeleo kwenye jimbo la Ubungo. akiwa kwenye mradi huo wa upanuzi wa barabara eneo la kimara amesema mradi huo ni kiungo muhimu kwenye ukuaji wa uchumi hivyo ni muhimu ukamilile kwa wakati.
Aidha RC Chalamila ametumia nafasi hiyo kuwahakikishia wananchi kuhusu ujio wa magari ya mwendokasi ambayo yamekuwa yakilalamikiwa na wananchi ambapo amesema Serikali imeshaandaa mpango wa kupata magari ya kutosha lakini pia kuwa na mtoa huduma zaidi ya mmoja badala ya kutegemea UDART pekee jambo ambalo litasaidia kuboresha huduma hiyo.
Kwa upande wa Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe Lazaro Twange ameeleza lengo la serikali kuamua kutanua barabara ili kupunguza msongamano wa magari huku Mhandisi wa TANROAD Mkoa wa Dar es salaam Beatrice Rweyemamu wakati akitoa taarifa ya mradi huo ameeleza namna changamoto ya misongamano inavyoathiri wananchi endapo mradi huo utachelewa kumalizika kwa wakati.
Hata hivyo Mkandarasi anaejenga barabara hiyo amesema miongoni mwa changamoto za ujenzi wa barabara hiyo ni kuwa bize kutumika kwa masaa mengi wawapo kazini lakini wanakwenda kuongeza kasi kwa kufanya kazi saa 24
Katika ziara hiyo RC Chalamila ametembelea mradi wa *Shule ya msingi msewe, kituo cha afya Makurumla na ujenzi wa barabara ya kimara ubungo* na baadae kufanya mkutano wa hadhara na wananchi kwenye viwanja vya TP sinza
Akiwa kwenye Mkutano wa hadhara RC Chalamila amesikikiliza kero za wananchi na kuzitolea majawabu papo hapo, ikiwemo kero ya uvamizi wa maeneo ya wazi, Maji taka, na changamoto za huduma za Afya kwa Wazee. ambapo ametoa rai kwa wakazi wa DSM kufanya kazi kwa bidii “Adui namba moja wa maendeleo ni kichwa chako mwenyewe tufanye kazi tuko kwenye Ardhi yenye baraka” Alisisitiza RC Chalamila