Home LOCAL MZEE BUTIKU AMPONGEZA RAIS SAMIA KWA KUTEKELEZA MIRADI MIKUBWA YA MAENDELEO 

MZEE BUTIKU AMPONGEZA RAIS SAMIA KWA KUTEKELEZA MIRADI MIKUBWA YA MAENDELEO 

Mwenyekiti wa taasisi ya Mwalimu Nyerere mzee Joseph Butiku,amempongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kutekeleza miradi mikubwa ya maendeleo,ikiwemo inayolenga kuongeza kasi ya ukuaji wa uchumi hapa nchini.

Thank you for reading this post, don't forget to subscribe!

Mzee Butiku ameyasema hayo ofisini kwake jijini  Dar es Salaam katika mahojiano maalum,ambapo amesema kazi kubwa ya utekelezaji wa miradi hiyo hasa ya sekta ya nishati,maji,elimu,afya,Reli na barabara katika kipindi cha miaka minne ya uongozi wa Rais Samia imewaziba midomo baadhi ya watu.

Amesema kuwa hakuna ubishi kuwa Rais Samia ameonesha utashi na mapenzi makubwa kwa taifa lake hasa katika kukamilisha miradi mikubwa ya kimkakati ukiwemo wa Reli,Bwawa la kufua umeme la Mwalimu Nyerere na ujenzi wa madaraja makubwa likiwemo la Busisi.

Amesema mbali na kutekeleza miradi hiyo mikubwa,serikali imesimamia vema katika suala la haki na usawa kwa kila mtanzania na kutoa uhuru wa watu kujieleza na kwamba,bado kuna tatizo kwenye eneo la maadili ambalo pia linahitaji nguvu ya pamoja kati ya serikali na wananchi.

“Hili la maadili hatuwezi kumtwisha mzigo Rais wetu,hili letu,wewe ni baba au mama una wajibu wa kutoa malezi katika familia yako,tukifanya hivi hata vitendo vya rushwa vitakwisha, mtoto anatoka chuo kikuu ananza kazi tu ananunua gari ya kifahari na kujenga nyumba nzuri,wewe mzazi unashangilia badala kumuuliza pesa hizo kwa mwaka mmoja tu amezitoa wapi kama sio mwizi” alisema mzee Butiku