Home LOCAL BALOZI DKT.NCHIMBI AZUNGUMZA NA WANANCHI NAMTUMBO

BALOZI DKT.NCHIMBI AZUNGUMZA NA WANANCHI NAMTUMBO

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi akizungumza na umati mkubwa wa wananchi Namtumbo, kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika Uwanja wa Shule ya Msingi Namtumbo, leo Alhamis tarehe 3 Aprili 2025.

Thank you for reading this post, don't forget to subscribe!

Katika mkutano huo, viongozi wa vyama vya ACT Wazalendo na Chadema, wakiwaongoza wanachama wao, waliamua kurejesha kadi na vifaa vingine vya vyama hivyo, kisha wakajiunga CCM.

Viongozi hao, akiwemo Ndugu Alifa Jafa, Mwenyekiti wa Chadema Wilaya ya Songea, Ndugu Mohamed Said Ndauka, Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Ntungwe na Azarius Lucas Ngonyani, Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Miembeni, walieleza jinsi ambavyo uongozi wa Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan na kuteuliwa kwa Balozi Nchimbi kuwa mgombea mwenza wa Urais, kwenye uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba 2025, umewavutia kuhamia CCM.