Home INTERNATIONAL RAIS WA MABUNGE DUNIANI IPU DKT. TULIA ACKSON AKUTANA NA BUNGE LA...

RAIS WA MABUNGE DUNIANI IPU DKT. TULIA ACKSON AKUTANA NA BUNGE LA SENETI LA MEXCO.

Thank you for reading this post, don't forget to subscribe!

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU), Mhe. Dkt. Tulia Ackson, leo tarehe 14 Machi, 2025 amekutana na kufanya mazungumzo Rais wa Bunge la Seneti nchini Mexico, Mhe. Gerardo Fernandez Norona na Rais wa Baraza la muunganiko wa Viongozi wa Vyama vyenye Uwakilishi kwenye Baraza la Uwakilishi la Mexico Mhe. Ricardo Monreal. 

Katika mazungumzo yao, Dkt. Tulia amewapongeza Viongozi hao kwa kuweza kuufikia usawa wa Kijinsia wakiwa na Wabunge wanawake wapatao asilimia 52.7 ya Wabunge wote wa Mexico. 

Aidha, Mexico ni miongoni mwa nchi 6 Duniani ambazo zimefanikiwa kufiki viwango vya juu vinavyolengwa vya usawa wa 50/50 wa uwakilishi wa Wanawake na Wanaume katika ngazi mbalimbali za Uongozi. Nchi nyingine zilizopo katika kumbi hilo ni Andorra, Nicaragua, Rwanda, Falme za Kiarabu na Cuba. 

Dkt. Tulia yupo nchini Mexico kushiriki Mkutano wa Kwanza wa Wabunge Wanawake wa IPU ambao unatarajiwa kufunguliwa tarehe 15 Machi, 2025 na Rais wa Mexico, Mhe. Claudia Sheinbaum.