Simba imerejea kwenye kilele cha Ligi ya NBC kwa kufikisha alama 47 baada ya kuwazaba Wajelajela, Tanzania Prisons kwa jumla ya mabao 3-0.
Mabao ya Simba yamefungwa na Jean Ahoua, Radack Chasambi na Elie Mpanzu na kufanya ubao usomeke 3-0 mpaka dakika 90 zinamalizika.
Nyota ya Chasambi imeng’aa upya baada ya kufunga bao na kurekebisha makosa aliyoyafanya kwenye mchezo uliopita ambapo alijifunga na kusababisha timu yake itoke sare ya 1-1 dhidi ya Fountain Gate.