Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Kassim Majaliwa akiwasili kwenye viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam kuaga mwili wa marehemu Jaji Werema.
Rais mstaafu Dkt. Jakaya Kikwete akiwa na Jaji Mkuu wa Tanzania Jaji Ibrahim Juma wakati wa kuaga mwili wa marehemu Jaji Fredrick Werema.
Wakili Mkuu wa serikali Dkt. Ally Possi akizungumza katika tukio hilo la kuaga mwili wa marehemu Jaji Werema.
Jaji mkuu wa Tanzania Mstaafu Jaji Mohammed Chande kushoto akiwa na Mwanasheria Mkuu mstaafubwa serikali Mh. Andrew Chenge wakati wa tukio la kuaga mwili wa marehemu Jaji Mstaafu Fredrick Werema kwenye ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam.
…………………..
Mwanasheria Mkuu wa Serikali mstaafu, Jaji Frederick Werema, alifariki dunia Desemba 30, 2024, katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) alipokuwa akipatiwa matibabu baada ya kuugua ghafla.
Jaji Werema alizaliwa mwaka 1955 na alifariki akiwa na umri wa miaka 69.
Ibada ya kuuaga mwili wake inafanyika leo Januari 2, 2025, katika Ukumbi wa Karimjee, Dar es Salaam. Ambapo waombolezaji mbalimbali wakiongozwa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Kassim Majaliwa.
Katika kipindi cha utumishi wake, Jaji Werema alihudumu kama Mwanasheria Mkuu wa Serikali kuanzia mwaka 2009 hadi 2014.
Kabla ya hapo, alikuwa Jaji wa Mahakama Kuu katika Divisheni ya Biashara na pia aliwahi kuwa Mwalimu wa Shule ya Sekondari Shaaban Robert kati ya mwaka 1979 hadi 1980.
Katika mahojiano, Jaji mstaafu Joseph Warioba alimuelezea Jaji Werema kama mtu mwaminifu, mkweli, na mwenye uadilifu mkubwa aliyetoa mchango mkubwa kwa nchi na dunia kwa ujumla
Rais Samia Suluhu Hassan alituma salamu za rambirambi kufuatia kifo cha Jaji Werema, akieleza kusikitishwa na msiba huo.
Kwa mujibu wa taarifa, mazishi ya Jaji Werema yanatarajiwa kufanyika Januari 4, 2025.
http://WAZIRI MKUU KUONGOZA WAOMBOLEZAJI KUAGA MWILI WA JAJI WEREMA KARIMJEE