Home BUSINESS TANZANIA NA JAPAN ZASAINI MKATABA KUENDELEZA KILIMO

TANZANIA NA JAPAN ZASAINI MKATABA KUENDELEZA KILIMO

 
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) (Katikati) na Balozi wa Japan nchini anayemaliza muda wake, Mhe. Yasushi Misawa (Kushoto), wakibadilishana Hati za Mkataba (Exchange of Notes) iliyosainiwa kati ya Serikali ya Tanzania na Ubalozi wa Japan, wakati wa hafla iliyofanyika katika Ofisi Ndogo za Hazina, jijini Dar es Salaam, ambapo katika hafla hio Dkt. Nchemba alisaini Hati ya Mkataba mwingine wa mkopo wenye masharti nafuu kati ya Serikali ya Tanzania na Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Japan (JICA) wa Yen za Japan bilioni 22.742 (sawa na shilingi bilioni 354.45), kwa ajili ya utekelezaji wa Mradi wa Uendelezaji wa Kilimo Vijijini unaojulikana kama “Agriculture and Rural Development Two Step Loan Project”, ambao utasimamiwa na JICA kwa niaba ya Serikali ya Japan na upande wa Serikali ya Tanzania utatekelezwa na Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB).
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) (Katikati) na Balozi wa Japan nchini anayemaliza muda wake, Mhe. Yasushi Misawa (Kushoto), wakionesha Hati za Mkataba (Exchange of Notes) iliyosainiwa kati ya Serikali ya Tanzania na Ubalozi wa Japan, wakati wa hafla iliyofanyika katika Ofisi Ndogo za Hazina, jijini Dar es Salaam, ambapo katika hafla hiyo, Mhe. Dkt. Nchemba, alisaini Hati ya Mkataba mwingine wa mkopo wenye masharti nafuu kati ya Serikali ya Tanzania na Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Japan (JICA) wa Yen za Japan bilioni 22.742 (sawa na shilingi bilioni 354.45), kwa ajili ya utekelezaji wa Mradi wa Uendelezaji wa Kilimo Vijijini unaojulikana kama “Agriculture and Rural Development Two Step Loan Project”, ambao utasimamiwa na JICA kwa niaba ya Serikali ya Japan na upande wa Serikali ya Tanzania utatekelezwa na Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB).
 
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) (Katikati aliyeketi) na Makamu wa Rais wa Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Japan (JICA), Bi. MIYAZAKI Katsura (kulia), wakisaini Hati za Mkataba wa mkopo kati ya Serikali ya Tanzania na JICA wa Yen za Japan bilioni 22.742 (sawa na shilingi bilioni 354.45), kwa ajili ya utekelezaji wa Mradi wa Uendelezaji wa Kilimo Vijijini unaojulikana kama “Agriculture and Rural Development Two Step Loan Project”, utakaosimamiwa na JICA kwa niaba ya Serikali ya Japan na upande wa Serikali ya Tanzania utatekelezwa na Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB). Wengine katika picha wanaoshuhudia tukio hilo ni Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Japan, Mhe. Fujii Hisayuki (wa pili kushoto aliyesimama), Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Cosato Chumi (wa pili kulia aliyesimama), Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Bi. Jenifa Omolo (wa tatu kulia aliyesimama) na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo (TADB), Bw. Frank Nyabundege.
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) na Makamu wa Rais wa Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Japan (JICA), Bi. MIYAZAKI Katsura, wakibadilishana Hati za Mkataba wa mkopo wenye masharti nafuu kati ya Serikali ya Tanzania na JICA wa Yen za Japan bilioni 22.742 (sawa na shilingi bilioni 354.45), kwa ajili ya utekelezaji wa mradi wa Uendelezaji wa Kilimo Vijijini unaojulikana kama “Agriculture and Rural Development Two Step Loan Project”, utakaosimamiwa na JICA kwa niaba ya Serikali ya Japan na upande wa Serikali ya Tanzania utatekelezwa na Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB).
 
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) na Makamu wa Rais wa Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Japan (JICA), Bi. Miyazuki Katsura, wakionesha Hati za Mkataba wa mkopo wenye masharti nafuu kati ya Serikali ya Tanzania na JICA wa Yen za Japan bilioni 22.742 (sawa na shilingi bilioni 354.45), kwa ajili ya utekelezaji wa Mradi wa Uendelezaji wa Kilimo Vijijini unaojulikana kama “Agriculture and Rural Development Two Step Loan Project”, utakaosimamiwa na JICA kwa niaba ya Serikali ya Japan na upande wa Serikali ya Tanzania utatekelezwa na Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB). (Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, WF, Dar es Salaam)
DAR ES SALAAM

Serikali ya Tanzania imetia saini mikataba miwili wa mkopo nafuu wa Shilingi Bilioni 22.742 kutoka Serikali ya Japan kupitia Shirika la Maendeleo la nchi hiyo, (JICA).

Akizungumza katika hafla ya utiaji saini mikataba hiyo iliyofanyika leo Januari 14, 2025 Jijini Dar es Salaam, Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba, amesema utekelezaji wa mikataba hiyo utawezesha ukuaji wa sekta ya kilimo kwa kuongeza uzalishaji kwa kupitia mitaji nafuu na kuwezesha wakulima kupata mikopo ya kati na yamuda mrefu.

Amesema vikundi mbalimbali vya uzalishaji pamoja na taasisi zinazojihusisha na kilimo zitawezeshwa kupata pembejeo bora na teknolojia ya kisasa na ya juu itakayowezesha kupata mazao mchanganyiko kwa kulima kilimo kinachohimili mabadiliko ya tabia nchi na kuchangia usalama wa chakula, maendeleo vijijini na uhimara wa uchumi kwa ujumla.

‘Kama mnavyofahamu kwamba Serikali ya Dkt. Samia Suluhu Hassan imetilia mkazo kwenye Kilimo Biashara, hii inatupeleka pia kufanya kilimo cha kisasa ambacho sio tu kwaajili ya chakula bali kibiashara, na pia Serikali ina dhana ya kujenga kesho iliyo bora inayolenga kuwapeleka vijana katika shughuli za uzalishaji hasa za kilimo kwa dhana pana inayojumuisha sekta nyingine ndogo inayojihusisha kwenye masuala ya kilimo’ amesema Dkt. Nchemba.

Aidha, amesema Tanzania imenufaika na ufadhili wa japani kwa miaka zaidi ya sitini katika sekta mbalimbali ikiwemo Kilimo, Afya, Maji, Nishati, Usafirishaji pamoja na elimu kupitia programu mbalimbali ikiwemo ya mkopo nafuu, nakwamba Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inatambua na kushukuru kwa ufadhili unaotolewa na Serikali ya Japan.

Dkt. Nchemba ameongeza kuwa mradi huo utasimamiwa na JICA kwa niaba ya serikali ya Japan, ambapo kwa upande wa Tanzania mradi utatekekezwa na Benki ya Maendeleo ya Kilimo (TADB).

Hafla hiyo iliyoshuhudiwa na Naibu Waziri wa Mamabo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Cosato Chumi, Naibu Waziri wa Mamabo ya Nje wa Japan, Mhe. Fujii Hisayuki, Balozi wa Tanzania nchini Japan, Mhe. Baraka Luvanda, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Bi. Jennifer Omolo na Mtendaji Mkuu wa Benki ya Maendeleo, (TADB), Bw. Frank Nyabundege, 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here