Na Mwandishi Wetu
MBUNGE wa Chalinze mkoani Pwani, Ridhiwani Kikwete ameongoza wananchi wa jimbo lake katika dua ya kumuombea Rais Samia Suluhu Hassan na kumshukuru Mungu kwa maisha, uhai, afya na neema aliyowapa kwa mwaka 2024.
Tukio hilo la dua ya kumuombea Rais Samia na kumshukuru Mungu kwa uhai, afya na neema limefanyika jimboni kwake Halmashauri ya Chalinze wilayani Bagamoyo mkoani Pwani ambapo imehudhuriwa na Rais wa Awamu ya Nne Jakaya Kikwete, masheikh na wananchi mbalimbali.
Kikwete ambaye ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Ajira, Kazi, Vijana na wenye Ulemavu wanamshukuru Mungu kwa katika maisha, uhai , afya na neema alizowajalia na kwamba sio ujanja wao ila ni kudra za Mungu.
“Tumemshukuru Mwenyezi Mungu kwa ajili ya Rais Samia na uongozi wake wenye mashiko na unaojali wananchi wake. Maendeleo tuliyoyapata, mafanikio yetu kama nchi, utulivu, amani na mshikamano uliopo yote ni kazi yake kwa neema na vipawa alivyojaliwa na Mwenyezi Mungu. Tunakushukuru zana Rais tunapoukaribisha mwaka mpya na kuendelea kukuombea Mungu,” amesema.
Kikwete aliwataka wananchi kumuombea kheri wazee, wazazi, watoto na wake zetu na kwamba Allah awape huruma, mapenzi , na malezi mema ili tuendelee kukua na kuleana pamoja.
“Tumeiombea nchi, kupatikane utulivu, idumu amani na upendo baina yetu. Tunamshukuru Mwenyezi Mungu kwa kila jema analotujalia. Mwenyezi Mungu atulinde sote na kutujalia amani na kuilinda Tanzania,” amesema.
http://RIDHIWANI KIKWETE, WANANCHI CHALINZE WAMWOMBEA RAIS SAMIA