Home SPORTS MBUNGI MECHI YA SIMBA Vs CS COSTANTINE KUTAZAMWA MWEMBEYANGA TMK

MBUNGI MECHI YA SIMBA Vs CS COSTANTINE KUTAZAMWA MWEMBEYANGA TMK

DAR ES SALAAM

Klabu ya wekundu wa Msimbazi Simba SC imetangaza viwanja vya mwembe yanga uliopo Temeke Jijini Dar es Salaam kama sehemu maalum itakayotumika kuangalia mechi yao yakumaliza hatua ya makundi dhidi ya CS Constantine utakaopigwa siku ya jumamosi Januari 18,2025 katika Dimba la Mkapa Jijini humo.

Taarifa hiyo imetolewa leo Januari 17,2025 na msemaji wa timu hiyo Ahmed Ally alipozungmza na wanahabari Jijini Dar es Salaam.

Ahmed amesema kuwa timu hiyo ina kazi kubwa ya kumaliza nafasi ya kwanza kwenye kundi lao, na kuwakumbusha wana simba wote kuhusiana na kuzuiliwa kuingia uwanjani, nakwamba limekuwa tukio la kuumiza kwani wapo mashabiki wengine  bado hawajaamini kile kinachoendelea.

“Adhabu hii ni mechi moja ambapo tukitumikia adhabu hii vizuri mechi ya robo fainali mashabiki wataingia uwanjani. Niwambe Wanasimba tuheshimu hii adhabu, mtu yoyote hata kama ni mjanja kiasi gani wa kuingia uwanjani, niwaombe Wanasimba kukaa mbali na Uwanja wa Mkapa kuna watu ambao watakuwa wanaangalia kama tumefata utaratibu.”

“Tuna idadi maalumu ya watu kuingia uwanjani hivyo hatazidi mtu hata mmoja. Kuna utaratibu tumepewa na CAF na sisi Simba tutaufata utaratibu huo. Kumekuwa na maoni mengi watu wakitaka tuweke screen kubwa kwenye uwanja wa Uhuru ili kelele zitakazopigwa ziwafikie wachezaji. Hairusiwi watu kukaa mita 1,000 kutoka uwanja wa Mkapa. Jambo hilo haliwezekani na kufanya hivyo ni kuvunja sheria.”

“Asiyehusika yoyote akae mbali na Uwanja wa Mkapa, najua tunaumia hata mimi mwenyewe naumia.”

“Kwa kuwa watu wanataka kuiona timu yao pamoja kama tulivyozoea, mdhamini wetu wa michuano ya kimataifa akaona atuandalie kitu cha kutuweka pamoja. Mo Cola ametutengea eneo maalumu la kukutana kuona timu yetu na eneo lenyewe ni Mwembe Yanga lililopo Temeke. Tutakuwepo pale kuanzia saa 5 asubuhi na kutakuwa na screen kubwa vibaya mno, hamjawahi kuiona.”

“Kutakuwepo na burudani mbalimbali siku hiyo kama mwimbaji wa nyimbo ya Wivu ambaye ni Dj Mushizo lakini pia atakuwepo Dj Sinyorita.”

“Lakini pia wiki mbili ziliopita tulizindua kampeni ya Onja na Ushinde ukinywa Mo Cola. Hivyo siku ya Jumapili Januari 19, 2025 kutakuwa na zoezi la kugawa zawadi kwa washindi na wengine watashinda pale pale.”

“Mimi binafsi Jumapili sitaenda uwanjani, taenda Mwembe Yanga. Nimeshazoea kelele hivyo takuwa na Wanasimba wenzangu kufurahia.”

“Kampeni ya Tunawajibika Pamoja hadi sasa tuna milioni 47,141,024. Zoezi letu litafungwa mara tu baada ya filimbi ya mwisho ya mchezo wa Jumapili. Tunaitafuta milioni 100 hivyo bado kama milioni 53.” Ahmed Ally.

 #WenyeNchi #NguvuMoja

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here