Home SPORTS YANGA YAICHAPA TANZANIA PRISONS KWA BAO 4 – 0.

YANGA YAICHAPA TANZANIA PRISONS KWA BAO 4 – 0.

YANGA leo imeendelea wimbi la ushindi baada ya kuifumua Tanzania Prisons kwa mabao 4-0 katika mechi ya Ligi Kuu Bara, huku Prince Dube akitupia bao moja na kumfanya afikishe matano kupitia mechi tatu mfululizo zikiwamo mbili za ligi na mojua ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Watetezi hao walipata ushindi kwenye Uwanja wa KMC Complex, ikiwa ni wa pili mfululizo tangu waanze kuutumia uwanja huo kutoka ule wa Azam Complex, na kuifanya Yanga irudi nafasi ya pili kutoka ya tatu ikiishusha Azam FC inayolingana nao pointi 33, lakini ikiizidi uwiano wa mabao.

Katika mchezo huo, kocha Sead Ramovic alikianzisha kikosi kilichokuwa na mabadiliko makubwa kulinganisha na kile kilichoifumua Mashujaa kwa mabao 3-2, akiwatumia nyota wa kigeni wa tatu, viungo Khalid Aucho na Stephane Aziz KI walioanza sambamba na Prince Dube, huku waliosaliwa wakiwa wazawa.

Ramovic alimpumzisha Abubakar Khomeiny aliyetunguliwa mabao mawili mechi iliyoopita na nafasi yake kuzibwa na Abutwalib Mshery, huku mabeki wote wakiwa wazawa akiwamo Kibwana Shomary na Nickson Kibabage sambamba na Ibrahim Bacca na Dickson Job, huku Clement Mzize, Mudathir http://YANGA YAICHAPA TANZANIA PRISONS KWA BAO 4 – 0.Yahya na Farid Mussa wakitumika eneo la mbele.

Washambuliaji walioanzishwa kwa pamoja, Clement Mzize na Dube kila mmoja alifunga bao na kuboresha vibubu vyao vya mabao kwa msimu huu.

Mzize alifunga bao la kwanza la Yanga kwa mchezo wa leo, dakika ya 13 akimalizia pasi ya Dube, likiwa la tatu kwake msimu huu, kabla ya Mzimbabwe huyo naye kufunga bao lake la nne kwa msimu huu, lililokuwa la tatu katika mchezo wa leo sekunde chache kabla ya mapumziko akimalizia pasi ya Aziz KI aliyeonekana kucheza kwa utulivu mkuu tofauti na mechi zilizopita, japo aliendelea kupoteza mipira mingi kabla ya kutolewa kumpisha Shekhan Ibrahim.

Mbali na Aziz Ki, wengine waliotolewa kipindi cha pili ni Khalid Aucho aliyempisha Duke Abuya, Dickson Job, Mzize na Farid nao walitolewa kuwapisha Pacome, Bakar Mwamnyeto na Chadrack Boka.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here