Home LOCAL WANANCHI WA KATA YA MNADANI WAENDELEA KUFANYA USAFI MWISHO WA MWEZI

WANANCHI WA KATA YA MNADANI WAENDELEA KUFANYA USAFI MWISHO WA MWEZI

http://WANANCHI WA KATA YA MNADANI WAENDELEA KUFANYA USAFI MWISHO WA MWEZI

Na. Coletha Charles, DODOMA

Wananchi wa Kata ya Mnadani Halmashauri ya Jiji la Dodoma walifanya usafi wa mazingira mita tano kuzunguka maeneo yao ya makazi na biashara ikiwa ni utekelezaji wa maelekezo ya serikali ya kila Jumamosi ya mwisho wa Mwezi.

Akizungumza wakati wa zoezi hilo la usafi, Mkuu wa Kitengo cha Usafi na Usimamizi wa Taka ngumu Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Dickson Kimaro, alisema kuwa ni wajibu wa viongozi kuhamasisha jamii juu ya umuhimu wa kuhifadhi mazingira na kufanya kazi kwa pamoja na wananchi.

Alisema kuwa wananchi wanatakiwa kujiepusha na utupaji wa taka ovyo katika maeneo na kufanya usafi katika mitaro ambayo inapitisha maji machafu kipindi hiki cha mvua nyingi na kujiepusha na mafuriko yatokanayo na uzibaji wa mitaro. 

Usafi ni ustaarabu ambao unaanza na mimi na wewe. Lakini katika kipindi hiki cha masika, kumekuwa na changamoto ya magonjwa mbalimbali ya kuhara na kutapika ambayo tunaweza kujiepusha kwa kufanya usafi kwenye maeneo yetu” alisema Kimaro.

Nae, Mkazi wa Mtaa wa Mailimbili, Mwadawa Omary, alimesa kuwa kila mwanajamii ana jukumu la kuhakikisha mazigira yanayo mzunguka yanakuwa safi kwa kushirikiana wanaweza kuboresha afya na ustawi wa jamii.

Usafi ni sehemu ya imani yetu na tunaposhirikiana, tunaweza kufanikisha malengo yetu ya kufanya maeneo yetu kuwa safi na salama. Ninaiomba halmshauri iwachukulie hatua watu ambao hawajitokezi kufanya usafi katika maeneo yao” alisema Omary.

Usafi wa Mazingira ni hatua ya kutekeleza maagizo ya serikali kuwa halmashauri zote nchini kila mwisho wa mwezi ziweze kufanya usafi kwaajili ya kuyatunza na kuweka mazingira safi na salama kwa ubora wa afya.

Previous articleHAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMAMOSI TAREHE 28,DISEMBA 2024.
Next articleAJALI YA GARI YAUA WATU SITA NYASA,WAMO WALIMU WANNE

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here