Home LOCAL UUNDAJI MAJUKWAA YA UWEZESHAJI WANAWAKE KIUCHUMI UANZE NGAZI YA VIJIJI NA MITAA...

UUNDAJI MAJUKWAA YA UWEZESHAJI WANAWAKE KIUCHUMI UANZE NGAZI YA VIJIJI NA MITAA – WAZIRI DKT. GWAJIMA.

Na WMJJWM-Dodoma

Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima amewataka Waratibu wa Majukwaa ya Uwezeshaji Wanawake Kiuchumi nchini kuzingatia Mwongozo mpya wa Uundaji na Uratibu hayo toleo la mwaka 2024 kwamba, uundaji utaanzia vijijini na kwenye mitaa kwa kutumia vikundi vya wajasiriamali.

Aidha, ameagiza Wataalam na Wenyeviti na Makatibu wa Majukwaa hayo ngazi ya Mikoa kuhakiki Vikundi vyote vya Wajasiriamali ngazi ya Kijiji/Mtaa na kuvipa hamasa ya kuunda majukwaa hayo.

Waziri Dkt. Gwajima ametoa maagizo hayo Desemba 18, 2024 jijini Dodoma wakati akifungua Mafunzo ya Awamu ya Pili kuhusu Mwongozo huo mpya kwa Waratibu na Viongozi wa Majukwaa hayo kutoka Mikoa 26 ya Tanzania Bara.

Waziri Dkt. Gwajima amesema, Mwongozo huo umekuja na maboresho yanayohitaji Majukwaa hayo yaundwe na Vikundi vya Wanawake Wajasiriamali ngazi ya Kijiji na Mtaa Ili kuepuka kuwa na Majukwaa yasiyogusa ngazi ya jamii.

Katika kuleta ufanisi wa Majukwaa haya, tumezingatia suala la Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa kuhakikisha zinawezesha utekelezaji wake hivyo, Waratibu wa Mikoa hakikisheni mnatenga fedha kwenye bajeti zenu kwa ajili ya uratibu wake.” amesema Waziri Dkt Gwajima

Naye Naibu Waziri wa Wizara hiyo Mhe. Mwanaidi Ali Khamis (Mb) amesema kuwa, Mwongozo huo mpya unalenga kuboresha uwezeshaji wa wanawake hivyo, viongozi hao wazingatie elimu watakayopata Ili kufanikisha Azma ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kuwainua wanawake kiuchumi.

http://UUNDAJI MAJUKWAA YA UWEZESHAJI WANAWAKE KIUCHUMI UANZE NGAZI YA VIJIJI NA MITAA – WAZIRI DKT. GWAJIMA.

Naye Naibu Katibu Mkuu wa Wizara anayeshughulikia Maendeleo ya Wanawake Bi. Felister Mdemu amesema, Serikali kupitia itaendelea kushirikiana na Wadau wote kuhakikisha Mwongozo huo unaeleweka na unazingatiwa.

Nao baadhi ya Waratibu na Viongozi wa Majukwaa hayo wameishukuru Serikali kwa kufanyia maboresho Mwongozo huo na kutoa Semina ya jinsi gani wanawake wa hali ya chini zaidi wataguswa na kuinuliwa kiuchumi.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here