Home LOCAL UTENDAJI KAZI WA RUHORO, RAIS SAMIA CHACHU YA WANA-CHADEMA KUTIMUKIA CCM NGARA

UTENDAJI KAZI WA RUHORO, RAIS SAMIA CHACHU YA WANA-CHADEMA KUTIMUKIA CCM NGARA

Viongozi na wanachama 6 wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Ngazi ya kata ya Muganza Jimbo la Ngara Mkoani Kagera akiwemo Tumain Petro ambaye ni Mwenyekiti BAVICHA wa Sasa wamejiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM) wakati wa tafrija ya Kusherehekea kukamilika kwa ujenzi wa Shule ya Sekondari ya Kata ya Nyamagoma huku chanzo kikiwa ni kasi ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo Jimboni humo.
Sherehe hiyo iliyofanyika Disemba 08, 2024 iliyodhaminiwa na Mbunge wa Jimbo hilo Mhe. Ndaisaba Ruhoro ambapo pamoja na mambo mengine wanachama hao walipata fursa ya kuzungumza na vyombo vya habari mara baada ya kukaribishwa CCM walieleza sababu zilizopelekea kuhama CHADEMA na kujiunga na CCM ikiwemo kuvutiwa na kazi na viwango vya uongozi Bora wa Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na Mbunge wa Jimbo la Ngara Mhe. Ndaisaba G Ruhoro ambaye ametekeleza ahadi zake alizozitoa kwa wananchi wakati alilokuwa akiomba kura mwaka 2020.
Miongoni mwa ahadi zake ilikuwa ni kujenga Sekondari, kujenga Minara miwili ya Mawasiliano na kufikisha umeme kwenye kata hiyo ahadi ambazo zimetekekezwa kwa asilimia mia moja.
Kwa takwimu za wazi zinaonyesha ahadi nyingi zilizotolewa na Mbunge Ruhoro zimetekelezwa kwa asilimia miamoja ambazo zilikuwa ni kujenga Sekondari, kujenga Minara miwili ya Mawasiliano na kufikisha umeme kwenye Kata hiyo.
Aidha Mbunge Ruhoro amewaomba wanachama wengine wa CHADEMA kuendelea kukiunga mkono na kujiunga Chama Tawala CCM ambacho ndicho chama sahihi chenye Sera, Ilani inayotekelezeka na viongozi wenye wekedi, utashi na uwezo wa kutatua matatizo ya wananchi ikiwemo kuleta maendeleo ya vitu na watu.
Naye Mwenyekiti wa CCM wa Wilaya ya Ngara Ndugu Vitalis Misago Ndailagije amewapongeza wanachama hao kwa kufanya uchaguzi sahihi wa kujiunga na CCM chama Tawala na kuwahakikishia kuwapa malezi bora na ushirikiano wa kutosha wakiwa wanachama wa CCM.
Previous articleMTENDAJI MKUU TARURA ATEMBELEA MAENEO YALIYOATHIRIWA NA MVUA JIJINI DODOMA
Next articleREA YAANZA KUTEKELEZA AGIZO LA SERIKALI LA KUSAMBAZA MAJIKO YA GESI WILAYANI 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here