Na Mwandishi Wetu
Tanzania kuzindua Tuzo za Utalii na Uhifadhi Disemba 20, 2024 mwaka huu kuenzi umahiri katika maeneo hayo.
Katibu Mkuu wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hassan Abbasi ameyasema hayo leo Jumapili Disemba 8, 2024, jijini Dar es Salaam alipokutana na waandishi wa habari na kueleza kuwa tuzo hizo zitazinduliwa jijini Arusha na zitapabwa na Burudani mbalimbali za kitaifa na kimataifa.
“Mwaka huu umekuwa wa mafanikio makubwa katika sekta ya utalii, hivyo Disemba 20 hatutazindua tuzo tu bali itakuwa siku yakusherehekea mafanikio katika sekta hii ikiwemo kushinda Tuzo ya World Travel Awards kama Kivutio Bora Zaidi Duniani Kwa Utalii wa Safari 2024,” alisema Dkt. Abbasi.
Amesema tuzo hizi zinalenga kuwaheshimisha wadau makampuni na pia wahifadhi ambao wamekuwa na mchango mkubwa katika kukuza sekta ya utalii na kuendeleza uhifadhi nchini.
http://TANZANIA KUZINDUA TUZO ZA UTALII NA UHIFADHI DISEMBA 20, 2024.