http://TAMASHA LA BIBI TITI LAFANYA YA KUENZI KAZI ZA SERIKALI
Na John Jayros
Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara, Mhe. John Mongella amesema Tamasha la Bibi Titi Mohamed siyo tu Tamasha linalotumika kumuenzi hayati bibi Titi bali ni Tamasha linalotumika kuenzi kazi kubwa inayofanywa na Serikali ya CCM inayoongozwa na Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Mhe. Mongella ameyasema haya leo Desemba 13, 2024 wakati akifungua rasmi tamasha lwa mwaka huu la Bibi Titi IKwiriri Wilayani Rufiji huku akimpongeza Mbunge wa Jimbo hilo Mhe. Mohamed Mchengerwa kwa kazi kubwa na nzuri anayoifanya ya kuwaletea maendeleo wananchi wa jimbo hilo.
Ametoa rai kwa viongozi wa CCM kote nchini kuendelea kushughulikia kero za wananchi na kuachana na kufikiria ushindi uliopita wa CCM badala yake kuendelea kuwaletea mandeleo
Kwa upande wake, Mhe Mchengerwa amemshukuru Mhe. Rais kwa kazi kubwa ya kuwaletea maendeleo wananchi wa Wilaya ya Rufiji huku akimpongeza kwa maono makubwa na mapinduzi makubwa aliyoyafanya katika kipindi kifupi cha uongozi wake.
“Naomba kuchukua nafasi hii kumshukuru Mhe. Rais kwa upendo wake kwa kuifanya Wilaya ya Rufiji kuwa Mamlaka ya Mji Mdogo hivyo kusaidia kunufaika na fedha za Benki ya Dunia” amefafanua Mhe. Mchengerwa
Katika ufunguzi huo, Halimashauri ya Wilaya ya Rufiji imetiliana saini mkataba wa ujenzi wa jengo la ofisi ya kisasa ya Wilaya hiyo lenye gharama ya zaidi ya Bilioni kumi.
Aidha, Mhe. Mchengerwa ametumia jukwaa hilo kuwahakikishia wananchi wa Rufiji kuendelea kutambua mchango wa hayati Bibi Titi na viongozi waliotangulia na kwamba atashirikiana nao katika kuwaletea maendeleo ya kweli
Amewashukuru umoja wa wanawake wa CCM kwa kuendelea kutambua mchango wa Bibi Titi na kuahidi kuendelea kuadhimisha kila mwaka.
Tamasha ya Bibi Titi Mohamed la mwaka huu ni la nne na limekuwa likiadhimishwa kwa kuelezea kazi kubwa inayofanywa na Serikali, ambapo kesho linafikia kilele chake.