Na. Faraja Mbise, DODOMA
MIAKA 63 ya Uhuru wa Tanzania Bara yavuka mikoa katika Jiji la Dodoma baada ya Muendesha Baiskeli kutoka Mkoa wa Kigoma, Wenseslaus Lugaya kuendesha baiskeli hadi Mkoa wa Dodoma ikiwa ni ushiriki wake katika Maadhimisho ya Miaka 63 ya Uhuru wa Tanzania Bara leo tarehe 9 Desemba, 2024.
Akiwa katika Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Lugaya alimkabidhi Bendera ya Taifa, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Rosemary Senyamule tukio lililoshuhudiwa na mamia ya wakazi wa Jiji la Dodoma wakiongozwa na mkuu wa mkoa.
Viongozi wengine walioshuhudia tukio hilo ni Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Alhaj Jabir Shekimweri, Kaimu Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma, Joseph Fungo na maafisa waandamizi wa serikali na sekta binafsi.