Home LOCAL NCHI ZA EAC NA SADC ZAAZIMIA KUENDELEZA TEKNOLOJIA YA MATUMIZI BORA YA...

NCHI ZA EAC NA SADC ZAAZIMIA KUENDELEZA TEKNOLOJIA YA MATUMIZI BORA YA NISHATI

*Ni katika Mkutano wa Kikanda wa Matumizi Bora ya Nishati (REEC 2024)*

*Dkt. Jafo asema maendeleo ya Viwanda yanategemea uwepo wa Nishati ya kutosha*

Mkutano wa Kikanda wa Matumizi Bora ya Nishati uliohusisha Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) na Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) uliomalizika leo jijini Arusha umetoka na maazimio mbalimbali yatakayowezesha nchi za EAC na SADC kuwa na Matumizi Bora ya Nishati.

Moja ya maazimio hayo ni kuendeleza kwa pamoja teknolojia za matumizi Bora ya Nishati ili kuweza kuwa na ufanisi katika matumizi ya nisbati.

Mkutano huo uliokuwa ukifanyika jijini Arusha tarehe 4-5 Desemba 2024 umefungwa na Waziri wa Viwanda na Biashara, Dkt. Selemani Jafo ambaye ameeleza kuwa umehusisha Watunga Sera, Sheria, Viongozi, Wataalam na Wabobezi katika masuala ya Nishati kwa lengo moja la kuwa na matumizi sahihi ya Nishati.

Dkt. Jafo amesema lengo la nchi ni kuendelea kukuza uchumi, viwanda vifanye kazi na biashara zifanyike kwa ufanisi lakini hilo litawezekana ikiwa kuna nishati ya kutosha ambayo uwepo wake unategemea usahihi katika matumizi yake.

Ameeleza kuwa, Tanzania inatilia mkazo suala la matumizi bora ya nishati ambapo kwa sasa Shirika la Viwango Tanzania (TBS) linaandaa viwango fanisi vya vifaa vya nishati vinavyozalishwa au kuingizwa nchi ambavyo vitawezesha nchi kutumia umeme kwa ufanisi.

Amemshukuru Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuwekeza katika miradi ya Nishati ambapo uwekezaji huo amesema kwamba una maana kubwa katika kuendeleza viwanda na biashara.

Aidha, ameishukuru Wizara ya Nishati kwa kuratibu Mkutano huo wa Siku mbili kwa kushirikiana na Umoja wa Ulaya (EU), Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) na Ubalozi wa Ireland.

Kwa upande wake, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Dkt. Khatibu Kazungu amesema Serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Nishati imejipanga kutekeleza Mkakati wa Matumizi Bora ya Nishati uliozinduliwa tarehe 4 Desemba 2024 kwa kuhakikisha Mkakati huo unatekelezwa kwa kuwekewa bajeti ili nchi iweze kuwa na ufanisi katika vifaa vya nishati.

http://NCHI ZA EAC NA SADC ZAAZIMIA KUENDELEZA TEKNOLOJIA YA MATUMIZI BORA YA NISHATI

Amesema kupitia Mkutano wa REEC 2024 maazimio mbalimbali yamefikiwa ikiwemo kufanya tafiti za pamoja ili kuboresha matumizi bora ya nishati na kuihusisha kikamilifu Sekta Binafsi.

kwa upande wake, Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu, Mhe.Selemani Kakoso amsipongeza Serikali kwa kuendesha na kusimamia mkutano wa REEC 2024 ulioleta mafanikio makubwa ikiwemo mafunzo na kubadilishana uzoefu ili kuwa na ufanisi kwenye matumizi ya nishati.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here