http://MTENDAJI MKUU TARURA ATEMBELEA MAENEO YALIYOATHIRIWA NA MVUA JIJINI DODOMA
#Atoa wiki mbili Kwa Mkandarasi kufanyia kazi mapungufu aliyoyabaini.
Dodoma
Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) Mhandisi Victor Seff amefanya ziara ya kutembelea baadhi ya maeneo yaliyoathiria na mvua zilizonyesha kwa siku mbili.
Katika ziara hiyo Mhandisi Seff alitembelea barabara ambazo zipo kwenye Mradi wa Uendelezaji wa Miji Tanzania Bara (TACTIC) katika maeneo ya Mkalama, Ilazo, Medeli na Swaswa-Mpamaa na kubaini mapungufu kadhaa.
Mradi huo wa TACTIC kwa Mkoa wa Dodoma unajenga barabara Km.10.19 na Mkandarasi ‘China Geo Engineering Corporation’ ambapo ilionekana amechelewa kutekeleza mradi huo na kusababisha athari eneo la Mkalama ambapo kuta za nyumba zimeanguka baada ya mvua kunyesha.
“Hadi sasa ni zaidi ya miezi 11 tangu aanze kazi hii lakini maendeleo ya kazi ni 35% badala ya 70%,namuagiza awasilisha mpango kazi wake na endapo sitoona mabadikiko ndani ya wiki mbili tutachukua hatua za kimkataba”.
Kwa upande mwingine Mtendaji Mkuu huyo alibaini mapungufu mengine ni kutokuweka tahadhari za usalama kwa watumiaji wa barabara wakati wa ujenzi kama mkataba unavyotaka.
Hivyo amemtaka mkandarasi huyo kuweka alama hizo pamoja na kuongeza kasi ya ujenzi wa barabara hizo kama alivyoagiza la watachukua hatua za kusitisha mkataba wake.
Aidha, Mhandisi Seff amebaini kuwa kazi za matengenezo za barabara mpya hazifanyiki kama inavyotakiwa na kwa wakati kinyume na maagizo aliyoyatoa Kwa Mameneja wote nchi mzima.
“Nasisitiza kwa Mameneja wote nchi nzima katika kipindi hiki cha msimu wa mvua,mkague madaraja na mifereji ili kuhakikisha kwamba inapitisha maji kama inavyotakiwa na kuepusha madhara kwa wananchi na uharibifu wa miundombinu ya barabara”.
Kwa upande wake, Meneja wa TARURA Mkoa wa Dodoma Mhandisi Edward Lemelo amesema kuwa wao kama TARURA Mkoa wameyapokea maelekezo ya Mtendaji Mkuu na kuahidi kuyafanyia kazi mara moja kwa kuanza na kazi ya uzibuaji wa makavati na mitaro yote yaliyozibwa na takataka ili kuruhusu maji ya mvua kupita na kuepusha athari kwa wananchi.