Home LOCAL LUTENI JENERALI HAJI OTHMAN AONGOZA KUAGA MWILI WA MEJA JENERALI BUSUNGU

LUTENI JENERALI HAJI OTHMAN AONGOZA KUAGA MWILI WA MEJA JENERALI BUSUNGU

http://LUTENI JENERALI HAJI OTHMAN AONGOZA KUAGA MWILI WA MEJA JENERALI BUSUNGU

Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania Luteni Jenerali Haji Othman ameongoza Maafisa Jenerali, Maafisa Wakuu, Maafisa wadogo, Askari na watumishi wa Umma kuuaga mwili wa aliyekuwa Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa marehemu Meja Jenerali Martine Busungu(Mstaafu) tarehe 27 disemba 2024, katika hospitali Kuu ya Jeshi Lugalo.

Marehemu Meja Jenerali Busungu(Mstaafu) aliwahi kushika madaraka mbalimbali yakiwemo Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa kuanzia 2018 hadi 2019. Mwili wa marehemu Meja Jenerali Busungu (mstaafu) aliyefariki tarehe 24 Disemba 2024 unatarajiwa kuzikwa kwa heshima za kijeshi siku ya Jumamosi tarehe 28 Disemba 2024,Nyegezi Jijini Mwanza.

Previous articleRAIS SAMIA ATOA ZAWADI KWA WAZEE,WATOTO NA WANANCHI MSIMU WA SIKUKUU.
Next articleDR. SAMIA JUMBE HOLIDAY BONANZA KUTIKISA SHINYANGA DESEMBA 31, ZAWADI NONO KUTOLEWA

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here