Home LOCAL KATIBU TAWALA KILIMANJARO KISEO AZINDUA TAMASHA LA SAME UTALII FESTIVAL NA KUTAJWA...

KATIBU TAWALA KILIMANJARO KISEO AZINDUA TAMASHA LA SAME UTALII FESTIVAL NA KUTAJWA KUCHANGIA KUKUZA UTALII WA SAME

http://KATIBU TAWALA KILIMANJARO KISEO AZINDUA TAMASHA LA SAME UTALII FESTIVAL NA KUTAJWA KUCHANGIA KUKUZA UTALII WA SAMENa Ashrack Miraji Fullshangwe Media 

Tamasha la utalii la Same Utalii Festival limezinduliwa rasmi wilayani Same, mkoani Kilimanjaro, na kutajwa kama chanzo cha kuibua na kutangaza vivutio mbalimbali vya utalii vilivyopo katika wilaya hiyo.

Tamasha hili pia limechangia kuhamasisha wawekezaji mbalimbali kuwekeza katika wilaya hiyo, ambapo awamu ya kwanza imepelekea wawekezaji watatu kujenga hoteli za kisasa za utalii.

Akizungumza leo kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Nurdin Babu, Katibu Tawala wa Mkoa huo, Kiseo Nzowa, alisema kuwa tamasha hili, ambalo mwaka huu linasherehekea awamu ya pili, limekuwa na manufaa makubwa kwa wananchi na taifa kwa ujumla.

Katibu Tawala Nzowa alisema kuwa, mbali na kutangaza vivutio vya utalii, tamasha hili limeongeza mzunguko wa biashara kwa wageni wanaofika wilayani Same kufanya matumizi, na pia limeongeza uelewa wa wananchi kuhusu masuala ya utalii.

Tamasha hili la Same Utalii Festival linasaidia kutangaza vivutio vya utalii vilivyopo wilayani Same, na pia limeweza kutambua rasmi vivutio hivyo kama mali kale na maeneo ya utalii,” alisema Nzowa.

Aliongeza kuwa, awali wilaya ya Same ilikuwa inatambulika kama wilaya isiyo na vivutio vya utalii, lakini kupitia tamasha hili, vivutio vingi vya utalii vilivyopo Same vimeonekana wazi.

Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Same, Kasilda Mgeni, alisema kuwa lengo la

tamasha hili ni kumuunga mkono Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika juhudi zake za kutangaza utalii kupitia kampeni ya Royal Tour, ambayo imeleta mafanikio makubwa kwa kuongeza idadi ya watalii nchini.

Kasilda alisisitiza kuwa, lengo jingine ni kuhakikisha kuwa vivutio vya utalii vilivyopo wilayani Same vinawanufaisha wananchi wa wilaya hiyo, pamoja na kuhamasisha uwekezaji kupitia sekta ya utalii.

Moja ya mafanikio makubwa tuliyoyapata kupitia awamu ya kwanza ni kuweza kupata wawekezaji watatu ambao wanajenga hoteli za kisasa tatu wilayani Same, jambo litakalosaidia kutoa ajira kwa vijana,” alisema Kasilda.

Aidha, Mkuu huyo wa Wilaya aliongeza kuwa idadi ya watalii wanaotembelea vivutio vya utalii vya Same imeongezeka mara mbili, na hivyo kuchangia kukuza vipato vya wananchi wa Same.

Previous articleTANZANIA, SAUDI ARABIA KUIMARISHA USHIRIKIANO SEKTA YA NISHATI
Next articleHAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMAMOSI TAREHE 21, DISEMBA 2024.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here