Home SPORTS GAVANA BWANKU AENDELEA KUGAWA MIPIRA KWA TIMU MBALIMBALI NDANI YA TARAFA YA...

GAVANA BWANKU AENDELEA KUGAWA MIPIRA KWA TIMU MBALIMBALI NDANI YA TARAFA YA KATERERO.

Afisa Tarafa wa Tarafa ya Katerero iliyopo Bukoba mkoani Kagera Ndugu Bwanku M Bwanku ameendelea kugawa mipira kwa timu mbalimbali za Kata ndani ya Tarafa ya Katerero ikiwa ni hatua ya kuunga mkono mkakati wa Serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan kuinua michezo na kukuza ajira zaidi kwa Vijana kupitia michezo.

Tayali mpaka sasa, Gavana Bwanku amegawa mipira kwenye timu za Kata ya Kishogo, Ibwera, Kemondo, Katerero huku taratibu za kugawa kwenye Kata zingine zikiendelea.

Hizi ni jitihada za makusudi za Gavana Bwanku kumuunga mkono Rais wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan aliyedhamiria kuinua michezo nchini kwa vitendo na si maneno. Tayali Serikali ya Rais Samia kwa muda mfupi imeongeza Bajeti ya michezo kwa zaidi ya mara 8 kutoka Bilioni 35 tu hadi sasa imefika Bilioni 285, kujenga Viwanja vya Kisasa vya michezo mkoani Dodoma na Arusha, kuvipa motisha vilabu vyetu na Timu ya Taifa ambapo kwa mara ya kwanza katika historia ya Tanzania Yanga na Simba vilifika Roba Fainali Kombe la Afrika kwa mwaka mmoja na mengine mengi.

Bila kusahau Serikali ya Rais Samia ilifanikisha kupatikana kwa mipira zaidi ya 1,000 kutoka FIFA kupitia TFF na kuigawa kwenye shule mbalimbali mikoa yote Tanzania ili kuinua michezo.

Kwa kazi hii kubwa ya Rais Samia, Gavana Bwanku ameamua kuunga mkono jitihada hizi kubwa za Serikali.

http://GAVANA BWANKU AENDELEA KUGAWA MIPIRA KWA TIMU MBALIMBALI NDANI YA TARAFA YA KATERERO.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here