Home LOCAL DOLA ZA KIMAREKANI MILIONI 104 KUSAIDIA KUKUZA USAWA WA KIJINSIA NCHINI –...

DOLA ZA KIMAREKANI MILIONI 104 KUSAIDIA KUKUZA USAWA WA KIJINSIA NCHINI – WAZIRI DKT. GWAJIMA

Na WMJJWM – Dar Es Salaam

Serikali ya Tanzania imetia saini ya mkopo wenye thamani ya Dola za Kimarekani Milioni 100 na Msaada wenye thamani ya Dola za Kimarekani Milioni 4 kutoka Benki ya Dunia ili kutekeleza Mradi uitwao PAMOJA wenye lengo la kuwawezesha Wanawake Kiuchumi na kutokomeza Ukatili wa Kijinsia.

Hafla hiyo ya utiaji saini imeongozwa na Waziri wa Fedha Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba pamoja Mkurugenzi wa Benki ya Dunia Nathan Belete na kushuhudiwa na Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima leo Desemba 12, 2024 jijini Dar Es Salaam.

Akizungumza baada ya kusainiwa kwa mkataba huo Waziri wa Maendeleo ya Jamii Wanawake Jinsia na Makundi Maalum, Dkt. Gwajima amesema tayari Tanzania imeshazindua Sera ya Taifa ya Jinsia na Maendeleo ya Wanawake (2023) na Mkakati wake ambapo, malengo ya mkopo huo yanatafsiri yaliyomo kwenye Sera hiyo.

Ameongeza kwamba mradi huo utatekelezwa kwa pande zote mbili za Tanzania Bara na Zanzibar ambapo, zitajengwa nyumba salama kwa manusura wa ukatili, vituo vya malezi na makuzi ya watoto wa umri wa awali, Ofisi za Maafisa Ustawi wa Jamii na Maendeleo ya Jamiii na vitendea kazi kwa Maafisa Ustawi.

Kwa upande wake Waziri wa Fedha Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba amesema, Wizara ya Fedha itashirikiana moja kwa moja na Wizara ya Maendeleo ya Jamii katika kuleta usawa wa kijinsia na kwamba, kusainiwa kwa mradi huo kutasaidia utekelezaji wa Sera ya Jinsia na Maendeleo ya Wanawake (2023) kwa kuwa maeneo ya kipaumbele ya mradi,ambayo ni kuwezesha wanawake kiuchumi, kuzuia na kukabiliana na vitendo vya ukatili wa kijinsia.

Naye Mkurugenzi Mkaazi wa Benki ya Dunia nchini Nathan Belege ameipongeza Serikali ya Tanzania kwa kuendeleza juhudi za kuleta usawa wa kijinsia, hivyo Benki ya Dunia itaendelea kutoa ushirikiano na Tanzania kwa ajili ya kuimarisha uchumi wa wanawake.

http://DOLA ZA KIMAREKANI MILIONI 104 KUSAIDIA KUKUZA USAWA WA KIJINSIA NCHINI – WAZIRI DKT. GWAJIMA

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here