Home LOCAL WAZIRI MKUU MGENI RASMI MKUTANO WA PAMOJA WA MAWAZIRI NA VIONGOZI WA...

WAZIRI MKUU MGENI RASMI MKUTANO WA PAMOJA WA MAWAZIRI NA VIONGOZI WA WHO

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa leo Novemba 21, 2024 ni mgeni rasmi katika mkutano wa pamoja wa Mawaziri na Viongozi wa juu wa Shirika la Afya Duniani kuhusu hali ya Utekelezaji wa Afya kwa Wote na Utayari wa Kukabiliana na Dharura nchini.

Mkutano huo ambao unafanyika katika Hotel ya Hyatt Jijini Dar es Salaam ni sehemu ya utekelezaji wa Azimio la Mkutano wa 73 wa Afya duniani uliofanyika mwaka 2020 kuhusu kutekelezaji kwa hiari mapitio shirikishi ya hali ya utekelezaji wa afya kwa wote na utayari dhidi ya dharura za kiafya kwa nchi wanachama wa Shirika la Afya Duniani (WHO).

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here