Home LOCAL WAZIRI MKUU AFANYA MAZUNGUMZO NA DKT. MEHMET

WAZIRI MKUU AFANYA MAZUNGUMZO NA DKT. MEHMET

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa leo Novemba 13, 2024 amefanya mazungumzo na Balozi wa Uturuki ambaye anamaliza muda wake Nchini Tanzania Dkt. Mehmet Gulluoglu, Ofisi ndogo ya Waziri Mkuu Magogoni jijini Dar es Salaam.

Katika mazungumzo yao Mheshimiwa Majaliwa amemsihi Balozi Mehmet kuendelea kuwa balozi mzuri wa Tanzania popote atakapokuwa sababu tayari anajua fursa za uwekezaji na utalii zilizoko nchini.

Kwa upande wake Balozi huyo ameshukuru Ushirikiano ambao ameupata kutoka Serikalini katika kipindi chake jambo ambalo limechangia kuimarisha Ushirikiano baina ya nchi hizo mbili.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here