Home BUSINESS TPA, BANDARI YA ANTWERP KUSHIRIKIANA KUBORESHA HUDUMA BORA

TPA, BANDARI YA ANTWERP KUSHIRIKIANA KUBORESHA HUDUMA BORA

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania ( TPA) Bw. Plasduce Mkeli Mbossa, tarehe 14 Novemba,2024. amekutana na kufanya mazungumzo na Naibu Waziri wa Ushirikiano wa Maendeleo na Misaada ya Kibinadamu kutoka Wizara ya Mambo ya Nje ya Falme ya Ubelgiji Mhe. Dkt. Heidy Rombouts na ujumbe wake, Makao Makuu ya TPA jijini Dar-es-Salaam.

Katika mazungumzo yao waligusia ushirikiano kati ya TPA na Bandari ya Antwerp ya Nchini Ubelgiji katika maboresho ya huduma za Kibandari kulingana na Mkataba wa ushirikiano wa Bandari hiyo na TPA katika ushauri elekezi wa kuyafikia mabadiliko chanya ya huduma za Kibandari hapa Nchini.

Aidha mazungumzo yao yamegusia nia njema ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika kuimarisha zaidi ushirikiano na Umoja wa Ulaya hususani kwenye Maboresho ya Bandari Nchini na Sekta ya Uchukuzi kwa Ujumla huku Bw. Mbossa, amemueleza Naibu Waziri Rombouts na Ujumbe wake kuhusu fursa zilizopo za Uwekezaji katika Bandari zote Nchini.

Mkutano huo ulihudhuriwa pia na Balozi wa Ubelgiji nchini Tanzania, Mhe. Peter Huyghebaert na Maofisa wa Serikali ya Ubelgiji. Ushirikiano wa maendeleo uliopo kati ya Tanzania na Ubelgiji, tarehe Novemba 14,2024 umetimiza miaka 40 tangu kuanzishwa kwake.

14 Novemba,2024T

PA HQ

Previous articleBALOZI NCHIMBI KUONGEZA WAOMBOLEZAJI MAZISHI YA KIBIKI LEO
Next articleSERIKALI YATOA TAKRIBANI SHILINGI BIL. 41 KUBORESHA MIUNDOMBINU SUA
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here