Home LOCAL TIGO KWASASA INAJULIKANA KWA YAS

TIGO KWASASA INAJULIKANA KWA YAS

Honora Tanzania Public Limited (“Tigo”) na Honora Tanzania Mobile Solutions Limited (“Tigo Pesa”), ambazo ni sehemu ya kampuni ya AXIAN Telecom Group zimetangaza mabadiliko makubwa ya chapa ambapo sasa Tigo inajukikana rasmi kama Yas, huku huduma zake za kifedha, Tigo Pesa, zikibadilishwa kuwa Mixx by Yas.

Hatua hii muhimu katika historia ya kampuni, na inaakisi azma yake ya kuendeleza ubunifu wa kidijitali na ujumuishaji wa Watanzania kwenye huduma za kifedha.

Mabadiliko haya ya chapa ni sehemu ya mpango mkakati wa AXIAN Telecom wa kuunganisha makampuni yake yote ya mawasiliano barani Afrika kuwa chini ya chapa moja, Yas na Mixx by Yas kama alama ya nguvu ya Pamoja na mafanikio.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Waziri Wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Jerry Slaa alisema uzinduzi huo utaunganisha nchi za kiafrika, unaendelea kuweka msingi wa utekelezaji wa uchumi wa kidigitali wa Taifa kwa ujumla.

Matumizi ya TEHAMA yanaongezeka na matumizi ya mtandao unaongezeka , uzinduzi huu utamsaidia mtanzania kuweza kuongeza mawasiliano”

“Moja katika kitu ambacho makampuni haya yanachangia ni asilimia 1.25 ya mapato yao ghafi ambazo pesa hizo zinaenda kwenye maeneo ambayo yasingepelekwa minara kwasababu hayana mvuto kibiashara” alisema

Kwa upande wake waziri wa ujenzi mawasiliano na uchukuzi Zanzibar Dokta khalid Salum Mohamed amesema kuwa hii ni moja ya hatua kubwa kwani nchi tano zitatumia na pia itaongeza wigo kwenye nchi za afrika na hii itasaidia kuimarisha uchumi wa kidigitali lakini pia itaongeza ajira kwa vijana wengi

Naye Mkurugenzi wa tigo pesa (mixx by Yas) Angelica Pesha alisema kuwa Hatua hiyo muhimu katika historia ya kampuni, na inaakisi azma yake ya kuendeleza ubunifu wa kidijitali na ujumuishaji wa Watanzania kwenye huduma za kifedha lakini pia Mabadiliko haya ya chapa ni sehemu ya mpango mkakati wa AXIAN Telecom wa kuunganisha makampuni yake yote ya mawasiliano barani Afrika kuwa chini ya chapa moja, Yas n a Mixx by Yas kama alama ya nguvu ya Pamoja na mafanikio.

Rostam Azizi, Mwenyekiti wa Bodi ya Yas Tanzania, alisema Yas na Mixx by Yas, zinalenga kuakisi maono ya kampuni ya kuwa kiini cha mapinduzi ya kidijitali barani Afrika. Kupitia suluhisho za kisasa za kidijitali na kifedha, chapa hizi mpya zinalenga kuboresha maisha ya mamilioni ya Watanzania na kutoa fursa mpya zisizo na kikomo.

Yas ni ishara ya nguvu tuliyonayo Afrika. Mabadiliko haya yanaonesha dhamira yetu ya kuendelea kuwekeza na kuleta mageuzi ya kidijitali nchini Tanzania, bara na Visiwani. Tukishirikiana na Axian Telecom Group, tumejipanga kutengeneza fursa mpya, kuhamasisha ubunifu, na kujenga mustakabali bora ulio na lengo la kuimarisha sekta ya mawasiliano.”

Hassanein Hiridjee, Mwenyekiti wa Bodi ya Axian Telecom Group, alisema:
Axian Telecom imekuwa katika safari ya kipekee ya kuunganisha watu barani Afrika kupitia chapa zetu. Kadri tunavyopanua wigo wa humuma zetu, tunaendelea kuyafikia maono yetu ya kuwa kampuni ya mawasiliano inayotoa hukduma kwenye nchi nyingi zaidi barani Afrika. Tunapozindua chapa mpya ya Yas, tunalenga kuunganisha bara hili kwenye fursa mbalimbali. Tunaamini Yas itaendeleza mafanikio na utamaduni wetu huku ikitoa suluhisho jumuishi na endelevu za kiteknolojia.”

Jerome Albou, Kaimu Afisa Mkuu wa Yas Tanzania, aliongeza:
Leo ni siku ya kihistoria kwa kampuni yetu. Kama Yas, tumejipanga kuwa mshirika wa maendeleo, tukiwapa nguvu wateja wetu na kuwahakikishia kuwa biashara zitastawi katika mazingira yenye ushindani mkubwa. Hivyo basi tutaendelea kuwekeza katika teknolojia za kisasa, huduma bora kwa wateja huku tukiendelea kuwekeza kwa vijana ambao ni msingi wa maendeleo ya baadaye ya Tanzania.”

Mbali na kuunganisha chapa zake za makampuni ya mawasiliano , Axian Telecom pia inaunganisha huduma zake za kifedha nchini Togo, Senegal, na Tanzania chini ya chapa ya Mixx by Yas . Lengo ni kuboresha uzoefu wa wateja kwa kushirikiana zaidi kati ya nchi hizi. Huduma za kifedha kwa njia ya simu za mkononi ni eneo muhimu la ukuaji kwa kampuni barani Afrika, ikibaki mstari wa mbele katika ujumuishaji wa kifedha.

Mabadiliko haya yanaonesha azma ya Axian Telecom Group ya kuendelea kuboresha huduma zake kwa kutumia teknolojia, ili kuwahudumia wateja wake vyema zaidi na kufanikisha maendeleo endelevu barani Afrika.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here