Home SPORTS TAWA YAITOA JASHO TPDC MCHEZO WA KUVUTA KAMBA (ME) SHIMMUTA

TAWA YAITOA JASHO TPDC MCHEZO WA KUVUTA KAMBA (ME) SHIMMUTA

Timu ya Pete (TAWA) yaonesha ubora mkubwa

Na Beatus Maganja.

Timu ya wavuta kamba ya wanaume ya Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA) imeendeleza ubabe katika Mashindano ya Mashirika ya Umma, Makampuni na Taasisi Binafsi (SHIMMUTA) yanayoendelea Mkoani Tanga baada ya leo Novemba 16, 2024 kuivuta timu shindani ya TPDC Kwa mivuto miwili Kwa nunge.

Mchezo huo ulioanza kwa mikiki na tambo za hapa na pale kutoka pande zote mbili huku mashabiki wa timu hizo wakichagiza kwa ushangiliagi wa hamasa, ulizidi kupamba moto baada ya filimbi ya mwamuzi kupulizwa kuashiria mchezo kuanza na timu zote kupimana ubavu Kwa kuvutana Kwa kamba.

Huu ni ushindi wa tatu mfululizo kwa timu hii ambao licha ya kuiweka pazuri kwenye msimamo, umeifanya iendelee kuwa tishio kwa timu shindani zinazopangwa kucheza nayo.

Akizungumza baada ya mechi Mchezaji wa timu ya wavuta kamba ya TAWA Chamganda Khamis amesema timu hiyo imejiandaa vyema msimu huu kushinda kila mechi iliyo mbele yao na itahakikisha inaongeza jitihada ili kuwa mshindi wa Kwanza na kuondoka na medali ya dhababu.

Wakati huo huo, Timu ya Pete ya TAWA leo imepoteza mchezo wake dhidi ya ARU Kwa kufungwa magoli 23 Kwa 22 , huu ukiwa ni mchezo wao wa Kwanza kupoteza tangu waanze mashindano haya.

Pamoja na kupoteza mchezo huo Timu ya TAWA imeonesha ubora na ushindani mkubwa kwa ARU kiasi ambacho muda wote ilikuwa ikishangaliwa na wa washabiki mbalimbali waliojitokeza kutazama mechi hiyo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here