Home LOCAL SERIKALI YATOA TAKRIBANI SHILINGI BIL. 41 KUBORESHA MIUNDOMBINU SUA

SERIKALI YATOA TAKRIBANI SHILINGI BIL. 41 KUBORESHA MIUNDOMBINU SUA

 

FARIDA MANGUBE, MOROGORO

Takribani shilingi bilioni 41 zimetolewa na serikali kupitia Mradi wa Elimu ya Juu kwa Mageuzi ya Kiuchumi (HEET) unaofadhiliwa na Serikali ya Jamhuri ya Munngano wa Tanzania kupitia Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kwa kushirikiana na Benki ya Dunia kwa ajili ya ujenzi wa majengo mapya saba ya SUA ili kuboresha mazingira ya kujifunzia na kuleta mageuzi makubwa katika utoaji wa elimu nchini.

Kati ya fedha hizo shilingi Bil 39.5 ni gharama za wakandarasi na shiringi Bil. 1.4 ni gharama za washauri waelekezi, ambapo katika Kampasi Mkuu ya Edward Moringe, chuo kitajenga majengo matano ambayo yataghalimu shilingi Bil. 19.2 majengo hayo yatahusisha jengo la taaluma litakaloweza kuchua watu 3500 kwa wakati mmoja.

Pia jengo la taaluma la Ndaki ya Uchumi na Stadi za Biashara litakalokuwa na ofisi za watumishi, vyumba vya semina na kumbi za mikutano zenye uwezo wa kuchukua wanafunzi 1000 kwa wakati mmoja, ujenzi wa maabara ya bioteknolojia, maabara jumuishi pamoja na maabara ya sayansi ya mimea vipando kwenye chumba.

Akizungumza katika hafla ya utiaji saini wa mikataba ya ujenzi kati ya Chuo kikuu SUA na wakandarasi watakaojenga majengo hayo iliyofanyika Kampasi Kuu ya Edward Moringe, Makamu Mkuu, Prof. Raphael Chibunda amesema mradi huo unalenga kuboresha mitaala kwa kuzingatia mahitaji ya soko la ajira na kuongeza ubora wa usimamizi wa elimu ya juu nchini hivyo mchango wa vyuo vikuu utaongezeka kwenye uchumi wa taifa.

Amesema katika Kampasi ya Solomon Mahlangu chuo kitajenga majengo mawili yanayoghalimu shilingi Bil.17.1 ambayo ni jengo la taaluma lenye uwezo wa kuchukua watu 3500 kwa wakati mmoja na hostel yenye uwezo wa kuchua wanafunzi 500 kwa wakati mmoja.

Mhandisi Hanington Kagiraki ni mratibu wa mradi wa HEET kutoka Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia ameitaka SUA kusimamia vizuri ujenzi wa mradi huo ukamilike kwa wakati kama ilivyoainishwa kwenye mkataba kwa kuzingatia gharama za mradi na ubora wa kimataifa.

“Tunatarajia tupokee majengo yakiwa yamekamika na kila ndani ndani vikiwemo vifaa, hostel ziwe na vitanda, madarasa yawe na viti na meza sio mnatukabidhi majengo yasiyo na kitu ndani, ambayo hatujui kama ni darasa, bweni au maabara, kama hakuna vifaa huwezi kutofautisha kati ya hosteli na darasa kwani kitakuwa ni chumba tu, sisi hatupendi kupokea vyumba” amesema Mhandisi huyo.

Awali akizungumza mara baada ya kushuhudia utiaji saini wa mikataba hiyo Mkuu wa mkoa wa Morogoro Mhe. Adam Malima amesema serikali ya mkoa itahakikisha inashirikiana na SUA katika kuhakikisha miradi huo unakamilika kwa wakati.

Mradi huo utakuwa na majengo tisa yenye vyumba vya madarasa, hosteli za wanafunzi, Maabara, karakana za uhandisi pamoja na ofisi za watumishi, unatarajiwa kuimarisha mazingira ya kujifunzia katika Kampasi Mkuu ya Edward Moringe na Kampasi ya Solomon Mahlangu zilizopo Manispaa ya Morogoro pamoja na kampas ya Mizengo Pinda iliyoko Katavi.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here